Baada ya kukamilisha maandalizi ya kiufundi na kimkakati: Atabatu Abbasiyya tukufu yafungua tawi lake linalo shiriki katika maonyesho ya vitabu huko Tehran awamu ya thelathini na moja…

Maoni katika picha
Maonyesho ya vitabu ya kimataifa awamu ya thelathini na moja yamefunguliwa Juma Tano (15 Shabani 1439h) sawa na (2 Mei 2018m) na kushiriki vituo vya usambazaji vya kiirani 2050 na vituo 132 vya kigeni, miongoni mwa vituo vya Iraq ni Atabatu Abbasiyya tukufu, kupitia taasisi zake za kitamaduni, kielimu na vituo vya uchapishaji, mwaka huu inashiriki ikiwa na aina mbalimbali za vitabu ilivyo chapisha, pamoja na ushiriki wa kielektronik, baadhi ya vitengo vinavyo shiriki vimesha wahi kupata ushindi katika mahafali za kimataifa.

Haya yalisemwa na Ustadh Jasaam Muhammad Saidi ambaye ni kiongozi wa tawi la Atabatu Abbasiyya katika maonyesho haya, ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua: “Tumechukua sehemu muhimu ndani ya eneo la maonyesho, tuna vitabu vikubwa vya majuzuu (mausua) na vitabu vya kawaida, pia tunatoa huduma ya ziara kwa niaba katika Ataba tukufu, na kuna shindano la kielimu linalo fanyika kila siku na matokeo yake yatatangazwa siku ya kufunga maonyesho haya, tumeandaa screen inayo onyesha video mbalimbali za matukio yanayo fanyika katika Ataba tukufu, na tumeandaa sehemu ya kutabaruku na bendera ya kubba la dhahabu la Abulfadhil Abbasi (a.s)”.

Akabainisha kua: “Watumishi wa Ataba tukufu wamekamilisha maandalizi yote ya kushiriki, ikiwa ni pamoja na kuleta vitabu kutoka Iraq, kuandaa mabango na kuyaweka, pamoja na kupanga vitabu. Tawi letu limepata mwitikio mkubwa tangu asubuhi mara tu baada ya ufunguzi wa maonyesho haya, tumekua na nafasi ya pekee kama tulivyo kua katika maonyesho yaliyo pita, kwa sababu vitabu tunavyo onyesha vimeandikwa na kuchapishwa na Ataba yenyewe na havipatikani sehemu zingine, jambo hili hutufanya tuonekane wa pekee katika maonyesho mengi tunayo shiriki ya kitaifa na kimataifa yakiwemo maonyesho haya.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha shiriki mara nyingi katika maonyesho ya kitaifa na kimataifa katika nchi mbalimbali, na imesha shiriki katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa ya Tehran mara nyingi, mara ya kwanza kushiriki maonyesho haya ilikua ni awamu yake ya ishirini mwaka wa 2007 miladiyya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: