Sababu ya kua na jamaa nyingi katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Maoni katika picha
Zaairu wa malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hususan katika usiku wa Ijumaa na katika ziara maalumu, anashuhudia swala nyingi za jamaa, na wala sio ile jamaa moja kubwa inayo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram tukufu peke yake, jamaa hizo huswaliwa wakati mmoja chini ya maimamu tofauti, baada ya kuongezeka idadi ya mazuwari pia zimeongezeka sehemu za swala za jamaa.

Ili kupata ufafanuzi kuhusu swala hili tumekwenda katika kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya na tumekutana na Sayyid Mudhar Qazwini ambaye ametuambia kua: “Hakika swala la kua na jamaa nyingi halikuanza leo, ni jambo la muda mrefu, haram zote mbili ya Imamu Hussein na Aulfadhil Abbasi (a.s) zinaswaliwa jamaa nyingi, hii ni kwa mujibu wa sheria tukufu na fatwa za wanachuoni wengi zimekubaliana kuhusu swala hili, swala ya jamaa ina masharti yake, miongoni mwa sharti muhimi ni kuwepo kwa mfungamano na Imamu wa jamaa, kutokana na udogo wa eneo la kuswalia ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi, na wingi wa watu wanao swali kunakua na ugumu wa kupatikana mfungamano na Imamu, hivyo inalazimika kuwepo na jamaa nyingi, miongoni mwa jamaa hizo ni:

Kwanza: Swala kuu ambayo huswaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) upande wa mlango wa Kibla.

Pili: Swala ambayo huswaliwa katika uwanja uliopo mkabala na mlango wa Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) nje ya haram tukufu.

Tatu: Swala ambayo huswaliwa katika barabara ya ubavuni mwa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) upande wa mashariki.

Nne: Swala ambayo huswaliwa katika Sardabu (ukumbi wa chini) ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Tano: Swala ambayo huswaliwa na wanawake katika Sardabu (ukumbi wa chini) ya haram tukufu –Sardabu ya Imamu Hussein na Imamu Haadi- (a.s)”.

Akaongeza kusema kua: “Swala hizi huswaliwa wakati mmoja na kila swala ina imamu wake, maimamu huo huchaguliwa kutoka katika watumishi wa kitengo cha dini, siku za mbele tunatarajia kuongeza sehemu za kuswalia ili kuwawezesha mazuwaru wengi kuswali jamaa, kwani hadi sasa wengi wao hawapati nafasi ya kuswali jamaa kutokana na udogo wa maeneo niliyo taja”.

Kuhusu maandalizi ya ziara za siku ya Ijumaa au ziara za siku maalumu amesema kua: “Kuna kazi kubwa ambayo hufanywa na vitengo vya Atabatu Abbasiyya tukufu, hususan kitengo cha dini na kitengo cha uangalizi wa haram, watumishi wa vitengo hivyo huanza kazi ya kuandaa sehemu zingine za kuswalia ikiwa ni pamoja na sehemu za Sardabu na kutandika miswala mapema ili kuwawezesha watu wengi zaidi kuswali jamaa”.

Mazuwaru huonyesha kufurahishwa na hatua hii inayo yanywa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kupata idadi kubwa ya mazuwaru kwenye swala ya jamaa, na namna zilivyo pangiliwa bila kuathiri harakati za mazuwari, pia wametoa wito kwa wenye mahoteli na maduka yanayo zunguka Ataba tukufu, kutoa ushirikiano kwa kupanua eneo la kuswalia kwa kiasi kinacho endana na idadi ya mazuwaru, ili waweze kufanya ibada zao na ziara kwa urahisi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: