Hivi punde kwa kielelezo: Marjaa dini mkuu atoa mwongozo kuhusu uchaguzi wa bunge la Iraq…

Maoni katika picha
Marjaa dini mkuu ametoa mwongozo kuhusu uchaguzi wa bunge la Iraq, ameonyesha msimamo wake kupitia khutuba ya pili ya Ijumaa iliyo swaliwa katika ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) leo mwezi (17 Shabani 1439h) sawa na (4 Mei 2018m) chini ya uimamu wa Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai, ifuatayo ni nakala ya khutuba hiyo:

Kutokana na kukaribia uchaguzi wa bunge, wananchi wengi wanauliza msimamo wa Marjaa dini mkuu kuhusu tukio hili muhimu la kisiasa, hivyo imetupasa kufafanua mambo matatu:

Kwanza: Tangu kuanguka kwa utawala wa kidikteta ulio pita, Marjaa dini aliona ni vizuri uingie utawala wa vyama vingi vya kisiasa, na kuwepo kwa utaratibu wa kubadilishana madaraka kwa amani kupitia masanduku ya kura, kwa kufanya uchaguzi huru, kutokana na ukweli kua hakuna njia nyingine bora kwa sasa ya kuongoza nchi, tukitaka mustakbali mzuri utakao mneemesha kila mwananchi na kujiona mwenye heshima na uhuru, na kulinda misingi ya utaifa na maslahi mapana.

Kutokana na hilo, Marjaa dini mkuu uliutaka utawala vamizi na umoja wa mataifa kufanya uchaguzi mkuu haraka na kuwapa fursa wananchi wa Iraq ya kuamua mustakbali wao wenyewe, kwa kuchagua viongozi wao, wakaanza kwa kuandika katika kisha wakachagua viongozi wa serikali ya Iraq.

Leo! Baada ya kupita miaka kumi na tano Marjaa dini mkuu bado anamsimamo uleule, mwenendo wa jambo hili unategemea uchaguzi sahihi unaolinda maslahi ya sasa na ya baadae, lazima kuwe na uangalifu wa kuingia katika maangamizi au utawala wa kidikteta kwa kisingizio chochote kile.

Ni wazi kua uchaguzi pekeyake haupelekei kupata matokeo mazuri ispokua kama utakamilisha masharti, miongoni mwa masharti ni: Sheria za uchaguzi ziwe za uadilifu, ziheshimu kura ya kila mtu wala isipatikane kura itakayo puuzwa. Sharti lingine: Wagombea washindane kwa kuelezea sera za uchumi, elimu na huduma zingine, waeleze mipango inayo tekelezeka, isiyo fungamana na ubaguzi wa aina yeyote. Sharti lingine: Uchaguzi usiingiliwe na watu wa nje, kwa kutoa pesa au vitu vingine na kuuwekea masharti. Sharti lingine: Wapiga kura wanatakiwa kua na uwelewa wa thamani ya kura zao na umuhimu wake katika kujenga mustakbali wa nchi, wasimpe kura mtu asiye faa kwa sababu ya kupewa kitu kidogo, au kwa ajili ya matamanio, mapenzi, au kwa maslahi binafsi au kutokana na kutoelewana kikabila na vinginevyo.

Ni wazi kua mapungufu yaliyo jitokeza katika uchaguzi ulio pita, yalipelekea utumiaji mbaya wa madaraka kwa wale walio chaguliwa na kupata nafasi za uongozi wa juu katika serikali, walifanya ufisadi na wakapoteza mali za umma kwa kiasi kikubwa mno ambacho hakijawahi kutokea, wakajipangia mishahara mikubwa mno, wakashindwa kutekeleza jukumu lao la kuwahudumia raia na kuhakikisha wanapata maisha mema, jambo hilo lilikua ni matokeo ya kawaida pale masharti ya uchaguzi yanapo acha kufatwa, hili tunaliona tena hivi sasa kwa namna moja au nyingine, lakini nafasi ipo ya kufanya marekebisho kutokana na uzalendo wa wananchi na kwa kutumia sheria.

Pili: Kushiriki katika uchaguzi ni haki ya kila raia aliye kamilisha masharti ya kisheria, hakina mwenye haki ya kumlazimisha kufanya maamuzi, anatakiwa afanye maamuzi yeye mwenyewe ya kumpa kura yule anaye muona kua atawanufaisha wananchi na taifa kwa ujumla, ndio.. inampasa azingatie ushauri wa watu wengine na awape nafasi na kuelezea mitazamo yao kuhusu mgombea wao na mwisho maamuzi yanabakia kwake mwenyewe, hatakiwi kulazimishwa katika maamuzi, na anatakiwa afanye maamuzi kutokana na uwelewa wake binafsi kwa kutanguliza maslahi ya taifa.

Tatu: Marjaa dini mkuu anasisitiza kua tangu mwanzo msimamo wake ni mmoja tu, haegemei upande wowote wala chama chochote, haungi mkono mtu yeyote, chama chochote wala mlengo wowote, mambo hayo anawaachia wagombea na wapiga kura, wachague yule watakaye muona anafaa, ni muhimu kuto ruhusu mtu yeyote au chama chochote kutumia jina la Marjaa dini mkuu kwa ajili ya kupata kura, jambo kubwa la kuzingatiwa ni uwezo wa mgombea na uaminifu wake, na kufuata misingi ya uchaguzi, pamoja na kujiepusha na ajenda za kigeni, na kuheshimu sheria, na kujiandaa kujitolea kwa ajili ya kunusuru taifa na kuwatumikia wananchi, pamoja na uwezo wa kutekeleza ahadi ya kuondoa matatizo yanayo wasumbua wananchi kwa miaka mingi.

Njia ya kuangalia uwezo wa wagombea ni kuangalia utendaji wao, hususan waliokua katika uongozi ulio pita, wasiwe ni wale walio ingia katika uongo na ufisadi, walio fanya maovu au mengineyo.

Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu aielekeze mikono ya watu wote katika watu wenye kheri na taifa, na wenye manufaa na wananchi hakika yeye ni muweza wa hilo na ni mwingi wa huruma mwenye kurehemu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: