Katika awamu ya tatu: Shule ya awali ya Saaqi yafanya mahafali ya kuhitimu wanafunzi (275)…

Sehemu ya mahafali
Kwa kushiriki wanafunzi (275) shule ya awali ya Saaqi ambayo ipo chini ya shule za Ameed, ambayo ipo chini ya kitengo cha malezi na elimu ya juu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, imefanya mahafali ya kuhitimu kizazi cha tatu cha wanafunzi wake, kizazi ambacho kimepewa jina la (Kundi la kuzaliwa kwa Muntadhir), mahafali hiyo imefanyiwa katika ukumbi uliopo katika jengo la Shekh Kuleini na kuhudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Ahmad Swafi na jopo la viongozi wa Ataba pamoja na wanafunzi.

Baada ya kusoma Qur’an ya ufunguzi pamoja na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, ulifuata ujumbe wa rais wa kitengo cha malezi na elimu ya juu Dokta Abbasi Rashidi Didda ambaye amesema kua: “Maendeleo wa watu hupimwa kwa kuangalia namna wanavyo jali malezi na elimu, hivyo Atabatu Abbasiyya tukufu imelipa umuhimu mkubwa sana jambo la malezi na elimu, kitengo cha malezi na elimu ya juu kumechukua jukumu la utendaji katika sekta hii, kimeandaa program maalum ya kulea watoto na ikaiita (Mfano wa mwezi), program hii imeonyesha mafanikio makubwa katika sekta ya elimu na michezo kwa kutoa wahitimu bora”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika michezo ya watoto ni muhimu sawasawa na wanafunzi wa rika zingine, kwani michezo humjenga mtoto kijamii na husaidia kuibua kipaji chake, pia humuimarisha kimasomo katika hatua zijazo, hivyo michezo inafaida kielimu, kijamii na kiafya, hukomaza fikra zake na hujenga uzalendo wa taifa lake, na mwanafunzi anapo fanya mahafali ya kumaliza hatua fulani ya masomo, humjengea kujiamini, na huhisi umuhimu wa hatua aliyo maliza na humsaidia kujiandaa kiakili kwa ajili ya kuingia hatua inayo fuata”.

Ratiba ya mahafali ikaendelea, baada ya ujumbe huo; likafuata tamko la ukaribisho lililo tolewa na mmoja wa wanafunzi wanao hitimu, halafu zikafuata kaswida na maigizo yaliyo fanywa na wanafunzi, kisha kikafuata kitendo cha kukabidhi bendera, ambapo wanafunzi wanao maliza waliwakabidhi bendera wanafunzi wanao india dara lao kama ishara ya kushika nafasi yao shuleni hapo kielimu, mwisho wa mahafali haya kulikua na maonyesho ya picha na vifaa vya kusomea.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: