Kamati imeweka masharti ya kushiriki katika shindano hilo kama ifuatavyo:
- 1) Mwisho wa kupokea mashairi yatakayo shiriki katika shindano ni (1 Jamadal-Thani 1440h) sawa na (07/02/2019m), shairi lolote litakalo pokelewa baada ya tarehe hiyo halita ingizwa katika shindano.
- 2) Lisiwe limekwisha shiriki katika shindano lingine.
- 3) Kila mtu ashiriki kwa kutuma shairi moja na lizingatie kanuni za mashairi ya kiarabu.
- 4) Lisiwe na beti zaidi ya (40) na sio chini ya (20).
- 5) Liandikwe kwa lugha fasaha ya kiarabu.
- 6) Maudhui ya shairi ihusu historia ya Imamu Hussein (a.s) au malengo ya harakati yake au izungumzie mafundisho yanayo patikana katika vita ya Twafu.
- 7) Nakala ya shairi iandikwe katika program ya (word) na itumwe pamoja na wasifu wa mwandishi utakao husisha vitu vifwatavyo:
- a) Majina matatu ya mwandishi.
- b) Sehemu na tarehe ya kuzaliwa kwake.
- c) Anuani na namba ya simu pamoja na barua pepe yake.
- d) Shahada (kiwango cha elimu).
- e) Fani aliyo somea chuo kikuu kama alifika huko.
- 8) Mashairi yatakayo shiriki katika shindano yawasilishwe kwenye kamati ya maandalizi ya kongamano la Rabiu Shahada, au yatumwe kupitia anuani maalumu ya kongamano.
- 9) Halitakubaliwa shairi lolote ambalo halita fuata masharti hayo hapo juu.
- 10) Nakala zote za mashairi hazita rudishwa kwa wahusika, na kamati ya maandalizi inahaki ya kuzitumia au kuzihifadhi.
Kiwango cha zawadi kwa washindi kitakua kama ifuatavyo:
Mshindi wa kwanza: (3,000,000) milioni tatu dinari za Iraq na midani ya dhahabu.
Mshindi wa pili: (2,000,000) milioni mbili dinari za Iraq na midani ya fedha halisi.
Mshindi wa tatu: (1.000,000) milioni moja dinari za Iraq na midani ya bronze.
Mshindi wa nne hadi wa kumi: (500,000) laki tano dinari za Iraq na cheti cha ushiriki.
Pia kutakua na zawadi tatu zingine kwa wale watakao soma vizuri zaidi mashairi katika kongamano. Tambua kua mashairi yote watakabidhiwa kamati ya majaji (watu walio bobea katika fani ya mashairi) watakagua kanuni za ushairi na ufasaha wa lugha.
Kwa maelezo zaidi wasiliana nasi kwa barua pepe ifuatayo: rabee@alkafeel.net au piga simu namba: (07801677644 / 07801863241).