Mwakilishi wa Marjaa dini mkuu afafanua jitihada alizo fanya kwa ajili ya islahi…

Maoni katika picha
Mwakilishi wa Marjaad dini mkuu Mheshimiwa Shekh Abdulmahdi Karbalai katika khutuba ya kwanza ya swala ya Ijumaa iliyo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) tarehe (17 Shabani 1439h) sawa na (4 Mei 2018m) alifafanua juhudi za kuleta islahi zilizo fanywa tangu mwaka (2003m) hadi leo, alisema kua:

Marjaa dini mkuu anatambua vyema harakati za kijamii katika sekta zote, na amekua akifuatilia mabadiliko na maendeleo yake, amekua daima akiitahadharisha jamii katika mambo yenye madhara kwa kutoa fatwa au tamko au kwa kupitia khutuba za Ijumaa, na amekua akiielekeza jamii katika mambo yenye maslahi.

Yalipotokea mabadiliko ya kisiasa ya mwaka (2003m) wakati ambao Iraq ilipita katika kipindi hatari cha kihistoria, alitoa maelekezo yaliyo saidia kuweka utaratibu wa kisiasa wa Iraq, akazingatia uwiano wa kidini, kimadhehebu, kijamii, na vielelezo vya kihistoria kwa kuangalia mazingira ya zamani na ya sasa, pamoja na athari za mazingira ya nje na vinginevyo, pia hakuacha kufuatilia maendeleo ya kisiasa na matukio yake, ameathiri kwa kiwango kikubwa mazingira ya Iraq, amekua akitoa nasaha na miongozo kwa lugha nzuri, akibainisha jambo la makossa na kuelekeza jambo sahihi, kama alivyo litazama kwa kina jambo la madhehebu katika jamii za wairaq.

Ametilia umuhimu mkubwa swala la kuishi kwa amani kwa tabaka zote za wairaq, na amefanya subira kwa yote yaliyo tokea miongoni mwa vitendo vya kigaidi vilivyo kua vikilenga raia kama vile magari yaliyo wekwa mabomu na kwenda kuribuliwa sehemu za makazi ya watu na mengineyo yaliyo pelekea kumwagika damu tukufu za wairaq.

Matunda ya kusubiri ni makubwa na muhimu nayo ni kulinda umoja wa Iraq,hatuwezi kusahau tukio kubwa la kihistoria sio kwa wairaq peke yao bali kwa nchi zote za kieneo, pale magaidi walipo vamia Iraq na wakateka theluthi nzima ya nchi, watu wakatahayari hawajui cha kufanya mauti imewakaribia, ikatolewa fatwa tukufu ya kujilinda, wakamiminika malaki kwa malaki ya wairaq kwenda kupigana kwa ajili ya kulinda nchi yao, mpaka walipo pata ushindi dhidi ya Daesh na kuwamaliza kabisa kilicho baki ni mabaki yao tu ya hapa na pale.

Hakika marjaa dini mkuu hajawahi kuacha jambo lenye hatari kubwa kwa taifa na raia wake ispokua atalitolea maelekezo tena kwa wakati unaofaa, lakini kazi ya islahi (kutengeneza) inafungamana na vitu vingi, inawezekana matokeo yakawa tofauti na alivyo taka mtengenezaji, na wakati mwingine matokeo huhitaji muda mrefu, hivyo ndio inavyo onyesha historia katika mataifa mengi, yampasa kila mtu ahisi majukumu katika kuleta mabadiliko na afanye subira katika safari ya kutengeneza.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: