Nadwa ya Qur’an: Maahadi ya Qur’an tukufu yafafanua manhaji ya kielimu ya Shekh Tusi katika tafsiri ya Qur’an…

Maoni katika picha
Katika mwendelezo wa nadwa za Qur’an tukufu, Maahadi ya Qur’an chini ya Atabatu Abbasiyya tayi la Hindiyya inafanya nadwa ya Qur’an kuhusu manhaji ya kielimu ya Shekh Tusi katika tafsiri ya Qur’an, nadwa hiyo imeendeshwa na Shekh Hussein Aali Yaasin ambaye ni Mu’tamad Marjaiyya katika mji mtukufu wa Kadhimiyya, katika mudhifu (mgahawa) wa Imamu Hussein (a.s) uliopo katika mji wa Hindiyya, na kuhudhuriwa na idadi kubwa ya walimu na watafiti pamoja na wanafunzi wa dini na wapenzi wa Qur’an.

Nadwa hiyo ilikua na uwasilishaji mzuri wa maudhui, ilijadili nukta mbalimbali za Qur’an, ikiwemo kutambulisha historia ya Shekh Tusi na elimu yake, kwa kujikita katika kitabu chake cha (Tibyanu fi ttafsiril Qur’an) na namna alivyo tilia umuhimu swala la kutafsiri kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, na manhaji yake ya kielimu iliyokua nguzo katika kati yeke tukufu, pamoja na nukta zingine kuhusu yeye binafsi.

Mwisho wa nadwa hii kulikua na michango, maoni na maswali mbalimbali, na Shekh Aali Yaasin alijibu maswali na kutoa ufafanuzi zaidi pale ulipo hitajika.

Mkuu wa tawi la Maahadi Sayyid Haamid Mar’abi amesema kua: “Miongoni mwa majukumu ya tawi la Maahadi katika wilaya ya Hindiyya ni kufanya nadwa na kutoa mihadhara mbalimbali kuhusu Qur’an tukufu, hua tunaalika wasomi wakubwa wa kisekula au wa kihauza, lengo letu na kufundisha utamaduni wa Qur’an tukufu na kubainisha elimu iliyopo ndani yake, sambamba na harakati zingine mbalimbali zinazo fanywa na Maahadi
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: