Katikati ya msongamano wa watu: Lafanyika shindano la kielimu na historia muhimu likisimamiwa na Atabatu Abbasiyya tukufu kwa ajili ya kuamsha ari ya kufanya utafiti…

Maoni katika picha
Wakati wa serikali ovu za Abbasiyya zilizo tawala Iraq kwa mabavu ndani ya muda wa miaka (534), walipotosha historia wakati wa utawala huo wa kidikteta.

Ukweli ulipotoshwa, wairaq wakatengwa, na wakajaribu kufuta nafasi yao katika vita ya Twafu, kwani wairaq ndio walikua idadi kubwa katika watu walio mnusuru Bwana wa Mashahidi (a.s), na wengine walizuiwa kwenda kumnusuru na jeshi la maadui ambalo asilimia kubwa ya wapiganaji wake walikua watu wa Sham, kama ilivyo pokewa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s).

Mwezi tisa Muharam ndio siku aliyo zungukwa Hussein (a.s) pamoja na maswahaba zake katika ardhi ya Karbala, “jeshi la wapanda farasi la watu wa Sham lilimzunguka, ibun Marjani na Omari bun Saadi walifurahishwa na kitendo hicho, na waliamini kua hakuna yeyote atakaye kuja kumnusuru Hussein miongoni mwa watu wa Iraq…” (Alkaaf – jz4 uk – h7).

Kwa hiyo imewalazimu wasomi wa Atabatu Abbasiyya tukufu kubainisha ukweli huu, kama sehemu ya kunusuru historia ya Imamu wao (a.s) na kubainisha ukweli kwa waumini, wamefanya hivyo kupitia shindano lililo andaliwa na Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zinazo shiriki katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Tehran awamu ya thelatini na moja, kama moja ya vitu ambavyo wamevifanya pembezoni mwa maonyesho hayo.

Haya ndio yaliyo semwa na Ustadh Jassaam Muhammad Saidi kiongozi wa kitengo cha machapisho ya Atabatu Abbasiyya katika tawi la Ataba, amesema kua: “Miongoni mwa maswali yaliyo ulizwa katika shindano la kielimu tulililo fanya yalikuwepo yanayo husu vita ya Twafu, na mengine yanayo husu maisha ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na historia ya Ataba mbili tukufu”.

Akabainisha kua: “Lengo la shindano hili ni kuamsha ari ya wasomi ya kufanya utafiti, pia tumewaelekeza watu walio tutembelea kua majibu ya maswali yote yaliyo ulizwa wanaweza kuyapata kupitia mitandao rasmi ya Ataba mbili tukufu ambayo ni (www.alkafeel.net) na (www.imamhussain.org) mitandao hiyo inataarifa rasmi za kihistoria, tawi liligeuka kua sehemu ya kiutafiti kwa kujibu maswali ya wadau, jambo hilo lilikua na athari nzuri hata kwa wasimamizi wa maonyesho”.

Kuhusu zawadi akasema kua: “Baada ya kumaliza maonyesho tutafanya kura ya majibu yote, ili hata yule aliye kosea anufaishwe na walio patia, zawadi zenyewe ni pete ya fedha iliyo tengenezwa na Atabatu Abbasiyya tukufu na kipande cha marumaru kutoka katika haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa washindi wa kwanza, na zawadi ya pili kwa wale ambao hawatapata bahati ya kupata pete ni kipande cha kitambaa kilicho fanyiwa tabaruku katika kaburi tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: