kituo cha Swidiqah Twahirah (a.s) chafanya hafla ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya…

sehemu ya hafla
Hafla ya kukumbuka kuzaliwa kwa miezi ya Muhammadiyya katika mwezi wa Shabani, ambazo huanza kwa kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hussein na huhitimishwa kwa kumbukumbu ya kuzaliwa mjukuu wake Muokozi wa wanadadamu Imamu wa Zama sambamba na kumbukumbu ya kuzaliwa Abulfadhil Abbasi, Imamu Sajjaad na Ali Akbar (a.s), kituo cha Swidiqah Twahira (a.s) –kinacho husika na harakati za kitamaduni na kielimu za wanawake- kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kimefanya hafla ya kukumbuka uzawa wa watu hao watukufu ndani ya ukumbi wake mkuu, na kuhudhuriwa na watu mashuhuri mbalimbali kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala.

Hafla ilifunguliwa kwa Qur’an tukufu na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehem mashahidi wa Iraq, kisha ukafuata ujumbe wa kituo hicho ulio wasilishwa na Ummu Sajjaad, alianza kwa kutoa pongezi kwa wahudhuriaji kutokana na mnasaba huu mtukufu, akabainisha kua: “Kutilia umuhimu matukio ya kidini ni sawasawa na maadhimisho mengine ya dini, kwa sababu yanalenga kukuza utendaji wa pamoja na utendaji wa idada pamoja na kuzienzi turathi za dini”.

Halafu ukafuata muhadhara ulio tolewa na Ummu Ali mkuu wa shule ya Faidhu Zaharaa (a.s), alizungumzia falsafa ya kusubiri na athari yake katika familia na jamii, na akaeleza nafasi ya vyombo vya habari vya kiarabu vya ndani katika jamii na vipi tunaweza kunufaika navyo katika kujenga uwelewa ndani ya familia kuhusu serikali ya Mahdi (a.f), akamaliza muhadhara wake kwa kuelezea sifa za kusubiri, miongoni mwa sifa hizo ni kua na tabia njema, pia alieleza kuhusu mimbari, na makhatibu wana jukumu gani katika kuifanya mimbari ya Husseiniyya kua sawa na mimbari ya Mahdawiyya.

Kisha zikafuata kaswida na maigizo kutoka kwa wanafunzi wa shule za Ameed za wasichana halafu watumishi wa mimbari ya Husseiniyya wakapewa zawadi.

Na mwisho kabisa ikapigwa kura ya shindano la (kuhifadhi wasia za Imamu Mahdi kwa Shia wake) shindano lililo lenga kuimarisha uwelewa wa wasia za Imamu Mahdi katika zama hizi za kumsubiri, ambapo yalitangazwa matokeo ya shindano lililo itwa (Jua lisilo zama).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: