Atabatu Abbasiyya tukufu yatoa mihadhara ya kubainisha maelekezo ya Marjaa dini mkuu kuhusu uchaguzi wa bunge…

Maoni katika picha
Baada ya maelekezo muhimu yaliyo tolewa na Marjaa dini mkuu katika mji wa Najafu kupitia mimbari ya swala ya Ijumaa inayo swaliwa ndani ya ukumbi wa haram ya Imamu Hussein (a.s) kuhusu uchaguzi wa bunge la Iraq, kumekua na uwelewa tofauti kuhusu maelekezo hayo pamoja na uwazi wa maelekezo hayo, kwa ajili ya kuchangia ufafanuzi wake na kulinda maelekezo yasipotoshwe na watu wenye nia mbaya, kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu kinatoa mihadhara ya kufafanua vipengele vilivyopo katika maelekezo hayo muhimu na ya kihistoria, ambayo yanaionyesha njia Iraq ya kujikomboa katika mazingira inayo pitia na kujiepusha kuwapa uongozi mafisadi.

Kwa mujibu wa maelezo ya rais wa kitengo cha dini Shekh Swalahu Karbalai aliyo uambia mtandao wa kimataifa Alkafeel, amesema kua: “Mihadhara hiyo inafanywa ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na hutolewa na mmoja wa watumishi wa kitengo cha dini miongoni mwa masayyid au mashekh watukufu kwa wazi mbele ya mazuwaru na watumishi”.

Akaongeza kusema kua: “Mihadhara hii inatolewa baada ya kuridhiwa na kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu, inalenga kuzuia maelekezo ya Marjaa dini mkuu yasipotoshwe na watu wenye nia mbaya wanao taka kuyatumia kwa maslahi yao na kujaribu kutoa ufafanuzi ambao hauendani na maelekezo yaliyo tolewa pamoja na uwazi wa vipengele vyote vitatu vilivyopo katika waraka wa maelekezo”.

Akabainisha kua: “Kutokana na maelekezo yaliyo tangazwa siku ya Ijumaa iliyo pita kutoka katika ofisi ya Mheshimiwa Sayyid Sistani, imetulazimu kuyafafanua kwa mazuwaru na watumishi pamoja na uwazi wa maelekezo hayo, hususan baadhi ya vipengele vinavyo changanya, kwa sababu ni haki ya raia kushiriki katika uchaguzi, jambo hili linahitaji kufafanuliwa vizuri”.

Akaendelea kusema: “Ndugu zetu watukufu siku hizi wanatoa mihadhara ya kufafanua maelekezo yaliyo tolewa na Marjaa dini mkuu kuhusu uchaguzi, tujitahidi kufafanua kila kipengele hadi vieleweke vizuri na watu wasichanganikiwe na kubadilisha ujumbe, haturuhusu mdau yeyote wa uchaguzi kukubali maelekezo fulani na kukataa maelekezo mendine, au kutumia maelekezo hayo waziwazi kwa ajili ya kujifanyia kambeni”.

Kumbuka kua Marjaa dini mkuu katika khutuba ya Ijumaa kupitia mimbari ya ukumbi wa haram tukufu ya Imamu Hussein (a.s) alitoa maelekezo kuhusu uchaguzi wa bunge la Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: