Waumini watuma ujumbe wa maandishi kwa Imamu Hussein na mbeba pendera wake (a.s), ukibebwa na watumishi wake kutoka Tehran hadi Karbala na kuwafanyia ziara kwa niaba…

Maoni katika picha
Mazingira ya upendo… na matumaini kwa Mola Mlezi… maombi ya shifaa ya Bwana wa Mashahidi Imamu Hussein na ndugu yake bwana wa kunywesha maji Abulfadhil Abbasi (a.s)…

Barua kutoka rohoni zilizo chapwa na zilizo andikwa kwa mikono, zimepokelewa na tawi la pamoja la Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa yanayo fanyika Tehran awamu ya thelathini na moja, barua hizo kuna ambazo zimeelekezwa katika kaburi la Imamu Hussein na zingine katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s).

Haya yameelezwa na kiongozi wa machapisho ya Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Jassaam Muhammad Saidi, ambaye alisema kua: “Tawi limeshuhudia watu wengi wakichukua karatasi na kuandika hisia zao”.

Akabainisha kua: “Kamati ya maandalizi ya makongamano na maonyesho ya kimataifa ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa karatasi maalumu za barua hizo, kuna karatasi za barua za kutumwa katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) na zingine ziliandaliwa na idara ya mikutano na makongamano ya kimataifa ya Atabatu Husseiniyya tukufu zinazo elekezwa katika kaburi la Bwana wa Mashahidi (a.s)”.

Akaongeza kusema kua: “Tumeandaa sanduku la pamoja kwa ajili ya kuweka barua hizo, idara ya tawi la maonyesho haya, baada ya maonyesho itabeba barua hizo kwa uaminifu mkubwa hadi Karbala, na kila barua itawekwa katika dirisha la kaburi kusudiwa za Ataba mbili tukufu, baada ya kuzichambua na kuziainisha kila moja imeelekezwa katika Ataba gani miongoni mwa Ataba mbili tukufu”.

Akafafanua kua: “Idara ya Massayyid ambao ni watumishi wa Ataba hizo kila moja itafanya ziara na kuswali rakaa mbili za ziara kwa niaba ya mwenye barua”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha shiriki maonyesho mengi ya kimataifa katika miji mbalimbali, na imeshiriki katika maonyesho ya kimataifa ya Tehran mara nyingi, kwa mara ya kwanza ilishiriki katika awamu ya ishirini ya maonyesho haya mwaka wa (2007m).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: