Idara ya maktaba ya kielektronic ya Atabatu Abbasiyya tukufu yaweka jiwe la msingi katika kuhifadhi mafanikio ya kielimu ya wairaq miongoni mwa kazi za wanachuo wa Iraq…

Maoni katika picha
Miongoni mwa kazi nzuri wanayo endelea kuifanya, ya kuhifadhi mafanikio ya kielimu na kuyaweka katika mikono ya watafiti na wasomi kwa ajili ya kunufaika nayo, idara ya maktaba ya kielektronic ambayo ipo chini ya maktaba na Daru Makhtutwaat ya Atabatu Abbasiya tukufu, imeweka jiwe la msingi katika kuhifadhi mafanikio ya kielimu yanayo patikana katika kazi za wanachuo wa Iraq, kwa kunufaika na uzowefu wa kubadilisha kutoka nakala za karatasi hadi kua nakala za kielektronic tena katika program za kisasa.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa maktaba ya kielektronic mradi huu unalenga mambo yafuatayo:

Kwanza: kuhifadhi mafanikio ya kielimu miongoni mwa kazi za wanachuo yasipotee, hususan kazi za muda mrefu ambazo zimesalia kwenye mashelfu.

Pili: kuziingiza katika mikonno ya watafiti kwa ajili ya kunufaika nazo kwa kufuata njia za kisasa zaidi za kielektronic ambazo ni rahisi.

Tatu: kueneza utamaduni wa kuzitunza kwa njia ya electronic katika taasisi husika.

Nne: kuchangia katika kuweka mazingira yanayo faa katika kuangalia mahitaji ya utafiti yanayo rahisisha kupata vielelezo vya kielimu.

Tano: kuendana na maendeleo ya kielimu yaliyopo katika sekta hii na kutumia muda mfupi katika utafiti.

Sita: kuandaa mazingira ya kurudisha elimu katika nafasi yake, baada ya kupita muda mrefu, na kuiweka katika mikono ya wanufaika na kuweka uwiyano wa kielimu.

Akaongeza kusema kua: “Mradi huu unahusika na kubadilisha nakala za kwenye makaratasi na kuzifanya kua nakala za kielektronic, tena kwa kiwango kikubwa cha ubora unao endana na maendeleo ya program ya (OCR) inayo tumika kusoma nakala katika sekta hii, katika hatua ya kwanza tumefanya mawasiliano na Darul Kutub na vielelezo vya kitaifa kwa ajili ya kuanzisha uwekaji wa namba katika kazi za wana chuo zilizopo katika makaratasi na ambazo hazijaingizwa kayika sistim ya electronic, baada ya hapo tukaelekea katika kuziboresha kazi hizo za wanachuo wa kiiraq, na tulianzia katika chuo kikuu cha Mustanswiriyya, ambapo tulikutana na kuandaa mkataba wa makubaliano ya kufanya kazi kwa ushirikiano, ufanyiaji wa kazi sehemu za makubaliano hayo ndio msingi wa kuanza kwa utekelezaji, baada ya chuo hicho vikafuata vyuo vingine, matkaba ya kielektronic imebeba jukumu la kunakili na kuweka namba katika kazi zisizo kua na nakala za kielektronic (za zamani na za sasa), baada ya kuibadilisha na kuiweka katika aina ya namba ndipo inarudishwa ikiwa imeambatanishwa na nakala ya kielekronic pamoja na kuihifadhi katika nakala za kielektronic”.

Akasema: “Kazi ya kubadilisha nakala za karatasi na kua za kielektronic inapitia hatua nyingi hadi kufikia hatua ya mwisho, ikiwa ni pamoja na hatua ya kusafisha, kupiga picha, kurekebisha, kutengeneza karatasi zilizo haribika na kuweka namba, hatua zote hizo zinafanywa na watalamu wa maktaba”.

Akamaliza kwa kusema kua: “Kopi ya kielektronic huhifadhiwa kwa kutumia program maalum ya kuhifadhi inayo endana na kazi husika, kupitia njia mbalimbali za kuhifadhi pamoja na uwezekano wa kuzitumia pale inapo kua hakuna haki ya usambazaji”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: