Kitengo cha malezi na elimu ya juu chahitimisha ratiba ya Mahdawiyya ya siku mia moja ya wanafunzi wa shule za Ameed…

Maoni katika picha
Tukiwa tunaishi katika kilele cha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa wanadamu Imamu Swahibu Asri wa Zamaan (a.f) na kwa ushiriki wa wanafunzi (300) kutoka katika shule za Ameed, kitengo cha malezi na elimu ya juu cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimekamilisha (ratiba ya Mahdawiyya ya siku mia moja), ilio dumu siku mia moja, na iliyo kua inalenga kumtambulisha Imamu Mahdi (a.f) kwa washiriki na itikadi kuhusu Imamu Mahdi sambamba na kupandikiza katika nafsi zao pamoja na kuifasiri kwa vitendo.

Hafla ya ufungaji iliyo fanyika katika ukumbi wa shule ya Qamar ilihudhuriwa na viongozi wa kitengo hicho pamoja na wawakilishi wa afisi ya malezi ya mkoa wa Karbala, baada ya Qur’an ya ufunguzi na kusomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq, ukafuata ujumbe kutoka kwa makamo kiongozi wa kituo cha malezi ulio wasilishwa na Dokta Mushtaqu Ali, akabainisha kua: “Atabatu Abbasiyya tukufu inafanya kila aina ya juhudi kutambulisha majukumu ya jamii kuhusu Imamu Mahdi katika kipindi hiki cha ghaiba, miongoni mwa program zao ni (program ya Mahdawiyya katika siku mia moja) iliyo simamiwa na shule za Ameed katika hatua ya pili, program hii imehusisha wanafunzi wa viwango viwili, ambao ni: wanafunzi wa kidado cha kwanza na kidato cha pili”.

Akabainisha kua: “Program hii inalenga kunufaika na muda uliopo baina ya swala mbili ambao ni kama dakika kumi, hutumiwa dakika hizo kuelezea majukumu ya waumini kuhusu Imamu wao katika wakati wa ghaiba, muda huo hutumika kuelezea moja ya jukumu au hadithi kutoka kwa Maimamu watakatifu (a.s), kisha wanafunzi hupewa maswali, pia hutumiwa siku ya Ijumaa kuziba mapungufu yaliyo tokea katika ratiba”.

Ratiba ya hafla iliendelea kwa kushuhudia maigizo yaliyo kua na mafundisho ya umuhimu wa kumtambua Imamu Mahdi (a.f), pamoja na kaswida zinazo fundisha uzalendo wa taifa na kuwapenda Ahlulbait (a.s), hali kadhalika yalifanyika mashindano baina ya shule zilizo shiriki, na mwisho wa hafla wanafunzi walio shinda wakapewa zawadi.

Kumbuka kua program ya Mahdawiyya husimamiwa na kituo cha malezi kwa wanafunzi wanao karibia kufikia umri wa kubalehe, kwa ajili ya kuwaeleza majukumu yao kwa Imamu wa zama zao, na vipi wanaweza kupambana na changamoto zilizopo katika jamii ya kiislamu na diniani kwa ujumla katika kipindi hiki cha ghaiba.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: