Kwa muonekano mzuri: Idara ya mawasiliano ya Atabatu Abbasiyya tukufu yamaliza maboresho ya mitambo ya kamera za haram tukufu…

Maoni katika picha
Ukamilisho wa uboreshaji wa mitambo yake na mwendelezo wa mafanikio, idara ya mawasiliano ya Atabatu Abbasiyya tukufu ambayo ipo chini ya kitengo cha miradi ya kihandisi imekamilisha maboresho ya mitanbo ya kamera za haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ubora wa hali ya juu.

Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa idara ya uhandisi, Muhandisi Farasi Abbasi Hamza: “Mradi huu ni sehemu ya kukamilisha miradi iliyo tangulia, pia ni sehemu ya kuendana na maendelea yaliyopo katika sekta ya teknolojia ya mawasiliano na ulinzi duniani, kutokana na umuhimu wa kutumiwa kwa teknolojia hiyo katika Atabatu Abbasiyya tukufu, tumejitahidi kuhakikisha mitambo ya kamera inayo tumika katika Atabatu Abbasiyya tukufu ina ubora mkubwa unao endana na maendeleo ya kisasa”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika mradi huu unalenga kuongeza uwezo wa mitango ya kamera za haram tukufu, kwa kuzibadilisha na kufunga kamera mpya (47) zenye uwezo wa hali ya juu”.

Akabainisha kua: “Hakika utekelezaji wa mradi huu ulikua na vipengele vingi, kwanza kulikua na kazi ya utambuzi na utafiti wa namna ya kutekeleza mradi, bila kuondoa sistim ya kamera za zamani, sambamba na kuondoa nyaya za zamani zilizo kua hazija onganishwa ndani ya haram tukufu, halafu ufungaji wa nyaya mpya na kuziunganisha na sistim mpya ya kamera zilizo ongezwa ili kuweza kuona kila sehemu ya haram, na kuweka sistim maalumu kwenye kamera za upande wa wanawake na upande wa wanaume”.

Mradi huu umepitia hatua zifuatazo:

Kwanza/ hatua ya usanifu: ulifanyika upembuzi yakinifu na ikaandaliwa taarifa kamili ya mradi na watalamu wetu watumishi wa kitengo cha uhandisi, kisha wakachagua sehemu mpya za kufunga kamera kwa ajili ya kuweza kuona sehemu zote za haram tukufu vizuri kushinda ilivyo kua awali.

Pili/ hatua ya kuweka mitambo: ilihusisha kuweka nyaya katika sehemu za kamera mpya kwa namna ambayo hazionekani, kisha kuweka kamera mpya katika maeneo yaliyo ainishwa na kurudia upangiliaji upya wa mitambo yote ya kamera.

Tatu/ hatua ya kupangilia: zimepangwa kamera maalumu upande wa wanaume na upande wa wanawake, pamoja na kuweka kamera mpya katika maeneo yanayo hitaji uangalizi zaidi, sambamba na kupanga kamera za kurekodi video na zile zinazo rusha picha katika screen kubwa.

Nne/ hatua ya utumiaji: ilijumuisha utumiaji wa sistim ya kamera za haram katika upande wa wanaume baada ya kumaliza kuziunganisha na haram kisha kamera na haram katika upande wa wanawake baada ya kuweka kamera maalumu kwa ajili yao, na kupangilia kamera zinazo rusha picha katika screen”.

Akamaliza kwa kusema: “Kazi imekalika ndani ya muda ulio pangwa kwa kutumia watalamu wa idara yetu, bila kusaidiwa na mtaalamu yeyote wa nje, siku za nyuma kazi hizi zilikua zinaigharimu Atabatu Abbasiyya tukufu pesa nyingi sana, baada ya kumaliza kufunga sistim hii tumeifanyia majaribio, imeonyesha mafanikio makubwa sana”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: