Mwezi mtukufu wa Shabani unao karibia kuisha unashindikizwa na tukio la kuhuzunisha, nalo ni uadui mbaya uliofanywa na Sadamu mwaka wa (1991m) katika kaburi la Bwana wa Mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), picha za uadui huo zimebaki katika akili za watu wa Marbala, zenye matukio mabaya ya kuliza, pale zilipo shambuliwa kubba mbili za haram mbili tukufu pamoja na milango yake na kuta zake kutoka angani na ardhini, mashambulizi hayo yalilenga kubba mbili na minara zake na sehemu kubwa ya haram kwa nje, mashambulizi ya anga yalisababisha kubomoka kwa kubba la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na sehemu kubwa ya ukuta wa uzio wa haram.
Makumbusho ya Alkafeel ya vifaa na nakala kale ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, kwa nafasi yake imeamua kuonyesha sehemu muhimu iliyo shambuliwa na utawala wa kidikteta uliopita kufuatia maandamano ya Shaabaniyya, miongoni mwa kumbukumbu walizo nazo ni sehemu za mabaki ya kubba tukufu la malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na vipande vya kuta na milango iliyo shambuliwa, hakika uadui ulio fanywa na utawala huo wa kidikteta umeacha athari ambazo ni ushahizi wa wazi wa unyama walio ufanya watu ambao hawakuheshimu maeneo matukufu wala utukufu wa watu wa nyumba ya Mtume (s.a.w.w).
Hakika vielelezo hivi vinaonyesha unyenyekevu wa watu wa Karbala katika kutunza alama za dini tukufu na wafuasi wa Ahlulbait (a.s) kwa ujumla duniani kote, watu walio uliwa kwa dhulma bila kuheshimu utu wao wala maeneo matukufu.
Kumbuka kua maonyesho ya Alkafeel ya vifaa na nakala kale ambayo yapo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, ni maonyesho ya kwanza miongoni mwa maonyesho ya Ataba za Iraq kufunguliwa, nayo ilifunguliwa mwaka wa (2009m) na bado inaendelea kuonyesha hazina yake kwa mazuwaru wa kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s).