Kwa lugha ya kiarabu, kiengereza na kifarsi: vyombo vya habari tofauti vyapongeza mafanikio ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa awamu ya thelathini na moja huko Tehran…

Maoni katika picha
Vituo vya luninga, redio na magazeti pamoja na mitandao ya kijamii ya Iran… vimetangaza zaidi habari za Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zinazo shiriki katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa awamu ya 31 huko Tehran.

Kiongozi wa kitengo cha machapisho ya Atabatu Abbasiyya tukufu, Ustadh Jasaam Muhammad Saidi amesema kua: “Vyombo vya habari vimeripoti matukio mbalimbali katika tawi letu, ikiwa ni pamoja na vitabu vyenye idadi kadhaa ya majuzuu (mausua) vilivyo chapishwa na Darul Kafeel, baada ya kuandikwa na kuhakikiwa na kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, walijikita katika kuripoti vitabu vilivyo pelekea Ataba tukufu ishinde katika maonyesha na mashindano yaliyo fanyika katika jamhuri ya kiislamu ya Iran ya kituo bora cha usambazaji, kikiwepo kitabu cha Urdibadi, Muhtasar wa habari mashuhuri, Twalibiyya na Maimamu kumi na mbili, na vinginevyo”.

Akaongeza kusema kua: “Qur’an tukufu iliyo chapishwa na Atabatu Abbasiyya ilivutia vyombo vya habari vingi vya Iran, kwani huo ndio msahafu wa kwanza kuchapishwa nchini Iraq kwa ukamilifu (kuanzia uandishi, usahihishaji, mpangilio na uchapaji) baada ya kuandikwa na mwandishi wa kiiraq bwana Hamid Saadi kwa mkono na akaupangilia na akasimamia kuchapishwa kwake katika Darul Kafeel ya kituo cha maarifa ya Qur’an tukufu kuichapisha na kuifasiri, chini ya Maahadi ya Qur’an katika kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu cha Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Akaendelea kusema kua: “Miongoni mwa vyombo vya habari vilivyo ripoti zaidi matukio ya tawi letu ni luninga ya Karbala, (Duu) ya Iran inayo tangaza kwa kifarsi na luninga ya Iran inayo tangaza kwa kiengereza (Press Iran) ambayo ilifanya mahojiano kwa lugha ya kiengereza na mkuu wa tawi kuhusu vitabu vinavyo shiriki katika maonyesho pamoja na mambo mengine ya kitamaduni yanayo fanywa na Ataba tukufu”.

Akaongeza kusema kua: “Idhaa za kiiran, magazeti na mitandao ya kielektronic ya Iran imefanya mahojiano mbalimbali kuhusu aina ya machapisho na vitabu vinavyo shiriki katika maonyesho, na kuhusu shindano linalo endeshwa ndani ya tawi hili pamoja na kipengele cha sanduku la barua za waumini zinazo tumwa katika makaburi matukufu, na mengineyo mengi miongoni mwa harakati zinazo fanywa na tawi hili”.

Akafafanua kua: “Ustadh Mukhtaru Muhammadi kiongozi wa taasisi ya utamaduni ya Iran inayo simamia magazeti na mitandao ya serikali ya Iran, alitembelea tawi hili na akaridhishwa na ushirikiano uliopo baina ya mtandao wa kimataifa Alkafeel na gazeti la Alwafaa la Iran linalo chapishwa kwa lugha la kiarabu, na kuhamisha habari kutoka katika toghuti ya kifarsi ya mtandao na kuziingiza katika toghuti zingine za kiiran, kumbuka kua mtandao unarusha habari karibu kila siku katika toghuti zake nane za lugha tofauti”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: