Kwa kushirikiana na kitivo cha habari katika chuo kikuu cha Dhiqaar: Atabatu Abbasiyya tukufu yasimamia warsha ya wanahabari…

Maoni katika picha
Ukumbi wa Imamu Hassan (a.s) uliopo ndani ya Atabatu Abbasiyya tukufu asubuhi ya Juma Tano (22 Shabani 1439h) sawa na (9 Mei 2018m), umekua mwenyezi wa warsha ya wanahabari, iliyo husisha wanafunzi na walimu wa kitivo cha habari kutoka chuo kikuu cha Dhiqaar, warsha hiyo imeendeshwa na kiongozi wa idara ya habari ya Atabatu Abbasiyya tukufu na rais wa wahariri wa jarida la (Swada Raudhataini) Ustadh Ali Khabaaz, warsha hii ni sehemu ya matunda ya ushirikiano uliopo baina ya chuo kikuu cha Dhiqaar na Atabatu Abbasiyya tukufu, katika kufundisha wanafunzi wa kitivo cha habari na kuinua vipaji vyao katika fani ya uandishi kwa kuwapa mafunzo ya vitendo tofauti na mafunzo ya nadhariyya wanayo pata katika masomo yao.

Ushirikiano huu na Atabatu Abbasiyya tukufu umetokana na uzowefu mkubwa walio nao katika sekta hii, pia kutokana na kujiweka wazi kwake katika taasisi na vituo vya habari, Ustadh Ali Khabaaz ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Warsha hii imefanyika kwa ajili ya kuwaonyesha wanafunzi wa kitivo cha habari tofauti ya kusoma kwa nadhariyya na kwa vitendo”.

Akaongeza kusema kua: “Sisi katika jarida la (Swada Raudhataini) kwenye kila mlango wa habari wa kitengo cha habari na utamaduni chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu tumekua na uzowefu mkubwa, kwa namna ambayo tunaweza kumuelekeza mwanafunzi misingi ya uandishi na namna ya kuyafanyia kazi yale aliyo yasoma kinadhariyya, wanafunzi wengi wanapo maliza chuo na wakaingia katika uwanja wa kufanya kazi, hukuta kuna tofauti kubwa baina ya kile walicho soma darasani na mazingira halisi ya kazi wanayo takiwa kufanya”.

Akasema: “Chuo kikuu cha Dhiqaar kimeichagua Atabatu Abbasiyya tukufu kua mahala pa kufanyia warsha hii kutokana na uzowefu mkubwa walio nao watumishi wa Atabatu Abbasiyya katika sekta ya habari walio upata kwa miaka mingi”.

Akamaliza kwa kusema kua: “Sekta ya habari ya Atabatu Abbasiyya tukufu tangu kuanzishwa kwake inamtafuta mwanahabari mahiri anaye fanya utafiti na mwenye uwezo mkubwa wa kutafakari”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: