Idara ya umeme iliyopo chini ya kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu: inafanya juhudi za aina yake katika kutengeneza umeme wa barabara zinazo elekea kwenye eneo hilo…

Maoni katika picha
Idara ya umeme iliyo chini ya kitengo cha eneo la katikati ya haram mbili tukufu, imekamilisha kazi ya kurekebisha taa zilizopo katika barabara zinazo elekea katika eneo hilo tukufu, kwa ajili ya kuboresha mazingira na kuweka njia mpya za umeme, pamoja na kuondoa nyaya zilizo zagaa za umeme mbadala (wa jenereta) zinazo haribu muonekano wa barabara hizo.

Kiongozi wa idara ya umeme katika kitengo cha katikati ya haram mbili tukufu Muhandisi Thaair Adhaar Shimri ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Hivi karibuni tumemaliza kazi mbalimbali, tumetengeneza upya njia za umeme unao elekea katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu, kuanzia barabara ya Kibla ya Imamu Hussein (a.s), barabara ya Kibla ya Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na barabara ya Hauraa (a.s), kama mnavyo fahamu barabara hizo ndio njia kuu za kuingia katika mji wa Karbala, na ndio zinabeba sura ya mji, hivyo tumejitahidi kuzikarabati na kuzifanya ziwe na muonekano mzuri, tumeweka taa, mapambo pamoja na kuondoa nyaya za zamani zilizo kua zimezagaa na kuharibu muonekano wa barabara na kuweka nyaya mpya”.

Akaongeza kusema kua: “Baada ya kumaliza matengenezo ya nje tulielekea katika barabara zinazo elekea katika haram mbili tukufu, kama vile barabara ya Imamu Ali (a.s) na barabara ya Imamu Swahibu Zamaan (a.f), tumemaliza kutengeneza na kupangilia nyaya katika barabara ya Imamu Ali (a.s), kazi bado inaendelea katika barabara ya Imamu Swahibu Zamaan (a.f)”.

Akamaliza kwa kusema kua: “Hakika uwekaji wa taa za barabarani na mapambo umefanyika kwa njia za kisasa zaidi, taa zilizo wekwa haziumizi macho kabisa”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: