Katika ushiriki wake wa nje ya nchi ya Iraq: Atabatu Abbasiyya tukufu yawanoa waumini kwa machapisho yake ya kielimu na kiakili katika kupambana na fikra potofu…

Maoni katika picha
Wimbi la vita ya kiutamaduni kwa vijana wanaoishi katika miji ya kiislamu ni kubwa, na hulenga kupunguza uwezo wa kutafakari na itikadi, jambo hilo limethibitishwa na watu wengi walio tembelea maonyesho ya vitabu ya thelathini na moja yanayo fanyika Tehran.

Haya yamesemwa na kiongozi wa machapisho ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika maonyosho hayo Ustadh Jasaam Muhammad Saidi, amebainisha kua: “Tawi la Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya lilikua kituo cha kila mwenye kutafuta uhakika, hasa kitengo cha machapisho ya Atabatu Abbasiyya, kitengo cha kiislamu cha masomo ya kimkakati ndani ya kitengo cha habari na utamaduni, kwa sababu kulikua na idadi kubwa ya vitabu vya falsafa sayansi na swarfu, vitabu vilivyo jaa dalili za kiakili na kinakili pamoja na hoja nyingi zinazo batilisha dalili za watu wanao kanusha kuwepo kwa Mwenyezi Mungu au dini”.

Akasema kua: “Vitabu hivi ni sawa na silaha iliyo mikononi mwa waumini inayo imarisha itikadi kuhusu Mwenyezi Mungu mtukufu na dini yake pamoja na Mitume wake, pia vitabu hivi vinafaida kubwa hata kwa wasiokua waislamu, kwani baadhi yake vimeandikwa na wasomi wa zamani wakiwemo wakristo, hivyo vijana wengi walikua wakimiminika kuangalia vitabu hivyo na wakaomba vifasiriwe kwa lugha ya kifarsi ili waweze kunufaika na wale wasio jua kiarabu, sambamba na kufungua tawi lingine la kiarabu”.

Akaongeza kusema kua: “Asilimia kubwa ya watu walio tembelea tawi hili ni viongozi wa kitamaduni, dini, shule na vyombo vya habari vya Iran vilivyo fanya mahojiano ya kina na viongozi wa tawi hili”.

Kamera yetu inakuletea sehemu ya picha za mahojiano hayo…

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imesha shiriki mara nyingi maonyesho ya kimataifa tena katika miji tofauti, na imeshiriki katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa ya Tehran mara nyingi, kwa mara ya kwanza ilishiriki katika maonyesho ya awamu ya ishirini mwaka (2007m).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: