Miongoni mwa matembezi anayo fanya kiongozi mkuu wa kisheria Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi katika vituo na taasisi zilizo chini ya Ataba, kwa ajili ya kuangalia utendaji wao na kutatua changamoto kama zipo, leo ametembelea Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) ya masomo ya hauza kwa njia ya mtandao chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya, ambayo makao makuu yake yapo katika mji wa Najafu na ndio kitovu cha miradi ya hauza kwa njia ya electronic.
Alipokelewa na kiongozi wa Maahadi Shekh Hussein Turabi pamoja na watumishi wa Maahadi hiyo, Shekh Turabi ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mheshimiwa hufanya ziara katika miradi na taasisi zilizo chini ya Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kukagua utendaji wao na kuangalia changamoto walizo nazo na kisha huangalia namna ya kuzitatua”.
Akaongeza kusema kua: “Katika ziara hii, ameangalia masomo ya kielektronic yanayo fundishwa hivi sasa, pamoja na ratiba ya baadae inayo tarajiwa kupanua wigo wa masomo ya hauza”.
Akaendelea kusema kua: “Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi amezungumzia vitu vingi, miongoni mwa vitu hivyo ni: Umuhimu wa nafasi ya Maahadi katika kutoa elimu ya Ahlulbait (a.s) kwa watu wa tabaka zote, hususan wale ambao ni vigumu kwao kujiunga moja kwa moja katika hauza za Najafu, kazi kubwa na muhimu inayo fanywa na hauza hii tukufu ya misafara ya kielimu na maarifa ya uislamu, pia amesisitiza umuhimu wa ikhlasi katika kazi na kuhakikisha wanafikia malengo ya kuanzishwa kwa Maahadi hii”.
Kumbuka kua Maahadi ya turathi za Mitume (a.s) ya masomo ya hauza ya kielektronic, ni kituo muhimu cha masomo ya hauza kwa njia ya masafa, inatoa masomo kwa wanafunzi wakiume na wakike kutoka nchi tofauti duniani, ambapo wanafundisha Fiqhi, Aqida, Tafsiri ya Qur’an, Hukumu za usomaji (Tajwidi), pamoja na elemu za lugha ya kiarabu na Mantiki, sambamba na semina za Fiqhi ya wanawake na ibaza ya Hija, pia wanafunzi hupata nafasi ya kujadili wao kwa wao na kubadilishana mawazo hali kadhalika kujadiliana na walimu wao.
Kwa maelezo zaidi piga simu ifuatayo: 07731881800