Uongozi mkuu wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya wafanya majlisi ya kumrehemu Jemedari Shekh Karim Khaqani (r.a)…

Maoni katika picha
Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya siku ya Ijumaa (24 Shabani 1439h) sawa na (11 Mei 2018m) zimefanya majlisi ya kumrehemu Shekh Karim Abdul-Hussein Khaqani (r.a) kamanda wa kikosi cha Imamu Ali (a.s), majlisi hiyo imefanywa katika moja ya sehemu zilizo pauliwa katika eneo la katikati ya haram mbili tukufu kwa ajili ya kukumbuka ushujaa aliyo kua nao marehemu katika vita vya ukombozi vilivyo piganywa chini ya uongozi wake.

Majlisi hiyo imehudhuriwa na kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya Mheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi pamoja na jopo la viongozi, na katibu mkuu wa Atabatu Husseiniyya Sayyid Jafari Mussawi na kundi kubwa la marafiki wa marehemu na wawakilishi wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji na kikosi cha Ali Akbaru (a.s), pamoja na vikosi vingine vya wapiganaji wa Hashdi Sha’abi vya ndani na nje ya mkoa wa Karbala, pia Shekh Twaahir Khaqani rais wa kamati kuu ya kusaidia Hashdi Sha’abi katika wakfu shia alihudhuria.

Kumbuka kua kamanda wa kikosi cha wapiganaji cha Imamu Ali (a.s) Shekh Karim Khaqani aliye kua mkuu wa brugedi ya pili ya Hashdi Sha’abi na kiongozi wa opresheni ya mashariki ya Ambaar, alifariki wakati akisafirishwa kwenda nje ya Iraq kuendelea na matibabu, alifanya kazi kubwa sana ya kukomboa maeneo muhimu kutoka katika udhibiti wa magaidi wa Daesh, pia alichangia sana kurudisha udhibiti wa jeshi la umoja katika maeneo yenye utata.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: