Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar amempongeza Muhandisi Yusufu Mahdi Shekh Raadhi kwa kuteuliwa kua katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya tukufu, amempongeza kwa kupata nafasi hiyo tukufu na akamuombea mafanikio katika utendaji wake, na aweze kuendeleza mazuri yaliyo anzishwa na walio mtangulia miongoni mwa ujenzi wa malalo tukufu ya Kiongozi wa Waumini (a.s).
Aliyasema hayo katika sherehe za kutawazwa kwake zilizo fanyika katika ukumbi wa Daru Dhiyaafa ndani ya Atabatu Alawiyya tukufu, iliyo hudhuriwa na rais wa wakfu shia Sayyid Alaa Mussawi, na kiongozi mkuu wa mazaru tukufu Sayyid Mussa Taqi Khalkhaali pamoja na makatibu wakuu na wawakilishi wa Ataba za (Husseiniyya, Kadhimiyya na Askariyya) na mazaru mbalimbali pamoja na jopo kubwa la wakuu wa vitengo vya Atabatu Alawiyya tukufu na ugeni rasmi wa kikabila na kijamii.
Rais wa wakfu shia Sayyid Alaa Mussawi amesisitiza kua: “Sehemu nyingi utendaji wa kazi unahitaji uzowefu, ikhlasi na ujuzi, na itakapo kua utendaji huo ni kutoa huduma katika sehemu ambayo imezungukwa na Malaika wa Mwenyezi Mungu mtukufu kinacho hitajika ni kushikamana na Mwenyezi Mungu, kwa sababu sehemu hizi sio maalumu kwa ziara peke yake bali suhemu hii inaangazia roho na fikra, leo ni siku tukufu sana katika mwezi wa Shabani na imezidi kua tukufu kwa kuteuliwa katibu mkuu mpya wa Atabatu Alawiyya ambayo ni Ataba tukufu sana, kwani ndani ya Ataba hii kuna kaburi la Bwana wa Mawasii, Kiongozi wa Waumini (a.s)”.
Naye katibu mkuu mpya wa Atabatu Alawiyya tukufu Muhandisi Yusufu Mahdi Shekh Raadhi alitoa shukrani zake kwa kusema kua: “Hakika jukumu hili kubwa na tukufu mno mlilo nipa sina budi kutoa shukrani zangu za dhati kwa Marjaa dini mkuu Sayyid Ali Husseini Sistani, natoa pia shukrani za dhati kwa Mheshimiwa rais wa wakfu shia Sayyid Alaa Mussawi kwa kunipa nafasi hii, ya kuniteua kua katibu mkuu wa Atabatu Alawiyya tukufu”.
Mwishoni mwa shughuli hiyo katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar akatoa zawadi ya kutabaruku kutoka katika malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s).