Hivi karibuni Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu imetoa kitabu cha kwanza kiitwacho (Tarajumu Rijali) chenye juzuu nne kilicho andikwa na Alamah Mhakiki Sayyid Ahmadi Husseini Ashkuri, hiki ni miongoni mwa vitabu vya Ilmu Rijaali (utambuzi wa watu), kimetaja watu ambao hawakutajwa katika vitabu vingine vya Ilmu Rijali au hawakuelezewa kwa ukamilifu kutokana na nafasi zao.
Rais wa kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu Shekh Ammaar Hilali amesema kua: “Kitengo kilianza uchapaji wa kitabu hiki na kukitoa katika muonekano mpya unao endana nacho, ili kutoa nafasi kwa wanafunzi wa fani hii, kuna vitabu vingi vya fani hii lakini kila kitabu kina sifa tofauti na kingine kuanzia ukubwa, mpangilio na rejea zake, ukirejea katika vitabu utathibitisha maneno yetu”.
Akaongeza kua: “Hakika leo kazi ya Mheshimiwa Mhakiki Alamah Sayyid Ahmadi Husseini Ashkuri ya kitabu chake cha (Tarajimu Rijali), aliyo ifanya chini ya mitihani mikubwa, kwanza kazi ya uandishi, pili kimekaa muda mrefu kikipigwa vumbi sasa wakati umetimia wa kunufaika na kilichomo, kimeandaliwa katika muonekano mzuri na hakuna anayejua nafasi yake ispokua anaye jua utukufu wake, hakika alitumia miaka stini akizunguka huku na kule, hadi alipo kuja kutoa mamia ya mistari na vitabu.