Kituo kimebainisha kua matangazo hayo yatapatikana kwa anuani zifuatazo:
SAT:INTELSAT 902@62°E
DL:11457.5V
SR:3000
DVBS2
8PSK
FEC 2/3
HD/MPEG-4
Ratiba ya urushaji wa matangazo itaanza karibu na mda wa Dhuhurain hadi baada ya swala ya Alfajiri, itakua na mambo mbalimbali, miongoni mwa mambo hayo ni:
- 1- Swala ya Adhuhuri na Alasiri saa (5:30) itarushwa kutoka katika Atabatu Husseiniyya tukufu.
- 2- Usomaji wa Qur’an tukufu saa (8:30) utarushwa kutoka katika Atabatu Husseiniyya tukufu.
- 3- Usomaji wa Qur’an tukufu saa (11:00) utarushwa kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
- 4- Swala ya Magharibi na Isha zikitanguliwa na kisomo cha Qur’an kuanzia saa (12:30) zitarushwa kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
- 5- Dua’aul-Iftitaah saa (2:00) jioni na itarushwa kutoka katika Atabatu Husseiniyya tukufu.
- 6- Muhadhara wa kidini saa (3:30) utarushwa kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
- 7- Mashindano ya Qur’an ya vikundi saa (5:00) yatarushwa kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
- 8- Dua’au Abuu Hamza Shimali saa (7:30) itarushwa kutoka katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
- 9- Dua za usiku saa (9:00) Alfajiri, zitarushwa kutoka katika Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya.
- 10- Swala ya Alfajiri saa (9:25) itarushwa kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu.
Matangazo hayo yatapambwa na picha za video kutoka katika malalo mawili matukufu na uwanja wa baina ya haram mbili, pia kutakua na program maalumu siku ya Juma Nne na Alkhamisi kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na vipengele vingine vinavyo husu kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s) na shahada ya Kiongozi wa Waumini (a.s), kituo kimefafanua kua; unaweza kufuatilia matangazo ya moja kwa moja kwa kutumia youtube.
https://www.youtube.com/channel/UCy0MMgRho_O8jxiIj46qMxw
Au kwa kutumia facebook.
https://m.facebook.com/alkafeel.for.artistic.production/
Kwa maelezo zaidi unaweza kupiga simu namba (009647706007187).