Kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu chafungisha zaidi ya ndoa (400) katika mwezi wa Shabani…

Maoni katika picha
Kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kua kimefungisha zaidi ya ndoa (400) katika mwezi wa Shabani, kilianza kufungisha ndoa baada ya kuingia mwezi wa Shabani kikaendelea hadi siku ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa binadamu Imamu Mahdi (a.f), ndoa hufungwa chini ya usimamizi wa Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na kuwaombea dua wana ndoa ya kuwatakia maisha mema yatakayo mfurahisha Mtume wao na watu wa nyumbani kwake watakasifu (a.s), na kuanza maisha ya ndoa kwa baraka za mwezi wa bani Hashim Abulfadhil Abbasi (a.s) na kwa baraka ya siku hizi tukufu.

Shekh Swalahu Karbalai rais wa kitengo cha dini cha Atabatu Abbasiyya tukufu ametuambia kuhusu kuongezeka kwa mwitikio wa kufunga ndoa katika mwezi huu mtukufu, amesema kua: “Hakika ufungishaji wa ndoa katika idara ya ndoa iliyopo ndani ya kitengo cha dini hufanyika kipindi chote cha mwaka ispokua miezi miwili, mwezi wa Muharam na Safar, hua kunakua na ongezeko kubwa la ndoa kipindi cha tarehe za kuzaliwa kwa maimamu (a.s) au minasaba ya kidini, na mwezi wa Shabani umejaa matukio hayo, basi idadi kubwa ya waumini hupenda kufunga ndoa zao katika mwezi huu mtukufu, tena katika Atabatu Abbasiyya chini ya kitengo cha dini, kwani kinatambulika serikalini, hivyo hupenda kufunga ndoa katika eneo tukufu, mwezi mtukufu na tarehe zenye matukio matukufu”.

Akaongeza kusema kua: “Hakika ufungishaji wa ndoa ndani miaka hii umeongezeka sana ukilinganisha na miaka ya nyuma, ukizingatia kua Iraq inasherehekea ushindi dhidi ya magaidi wa Daesh walio athiri kwa kiwango kikubwa ufungaji wa ndoa, harakati za kufunga ndoa hua nyingi katika tarehe za kuzaliwa kwa miezi ya Shaabaniyya, kwa ajili ya utukufu wa siku hizo ambazo ni siku za furaha kwa Mtume Muhammad (s.a.w.w) na watu wa nyumbani kwake (a.s)”.

Akabainisha kua: “Idara huanza kukutana na watu wanaotaka kufunga ndoa kuanzia asubuhi, asilimia kubwa ya watu wanaofunga ndoa katika mwezi huu hua wanakua waliahirisha ufungaji wa ndoa yao kwa ajili ya kusubiri mwezi wa Shabani uingie, na wala sio watu wa Karbala peke yake, kuna watu wanakuja kutoka mikoa mingine pia, sambamba na kufunga ndoa pia hupewa nasaha za maisha ya ndoa, kwa mujibu wa mafundisho ya dini ya kiislamu na mwenendo wa Ahlulbait (a.s)”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: