Matarajio ya kuandama mwezi mtukufu wa Ramadhani kwa mujibu wa maktaba ya Mheshimiwa Marjaa dini mkuu Sayyid Sistani…

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani inatarajia kuandama mwezi mtukufu wa Ramadhani jioni ya Juma Tano (29 Shabani 1439h) sawa na (16 Mei 2018m) katika anga la mji wa Najafu Ashrafu, wakati wa kuzama jua saa (12:53) jioni, kwa kiasi cha muinuko wa daraja (11) na dakika (41), utaendelea kuonekana baada ya kuzama jua kwa muda wa (saa 1) na (dakika 1), kiwango cha mng’ao wa mwezi kitakua ni (%1,96) katika mazingira hayo mwezi unatarajiwa kuonekana wazi.

Yamesemwa haya kwa mujibu wa nyakati za mwezi mwandamo kwa kuangalia mwezi wa Ramadhani wa mwaka (1439h) sawa na (2018m), iliyo rushwa katika toghuti ya ofisi ya Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani katika mji wa Najafu Ashrafu.

Kutokana na matarajio hayo, siku ya kwanza ya mwezi wa Ramadhani wa mwaka (1439h) itakua ni Alkhamisi sawa na (17 Mei 2018m) katika nchi ya Iraq na mashariki ya kati kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: