Kamati ya maandalizi ya kongamano la kitamaduni awamu ya kumi na moja la kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) yatangaza tarehe ya kuanza kwake…

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) awamu ya kumi na moja imetangaza tarehe ya kuanza kwa kongamano hilo, ambapo linatarajiwa kuanza mwezi kumi na nne Ramadhani hadi mwezi kumi na sita katika viwanja vya mazaru ya muujiza wa kurudisha jua (Radu Shamsi) –wa Imamu Ali (a.s) katika mkoa wa Baabil- mji wa Hilla.

Kongamano litasimamiwa na kamati kuu ya miradi ya Hilla, mji wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kwa kushirikiana na uongozi wa wakfu shia wa mkoa wa Baabil chini ya ulezi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya tukufu.

Mjumbe wa kamati ya maandalizi na naibu rais wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Aqiil Abdul-Hussein Yasiri ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Kongamano hili litafanyika kwa mara ya kumi na moja mfululizo chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Hassan (a.s) ni muokozi wa waislamu na mbainishaji wa uovu wa wanafiki), kongamano hili linafanywa kwa ajili ya kuadhimisha kuzaliwa kwa mjikuu wa Mtume mtukufu (s.a.w.w) Imamu Hassan Almujtaba (a.s), katika kongamano huli huzungumzwa historia yake na baadhi ya harabati zake, pia huwasilishwa tafiti mbalimbali zinazo husu uhai wa Imamu Hassan (a.s), hufanyika pia maonyesho ya vitabu, picha za mnato na za kuchora, pamoja na kutoa zawadi kwa wanachuoni wa Hilla, hua kuna visomo vya Qur’an na mashairi kwa muda wote wa siku tatu ambao ndio muda wa kongamano hili”.

Akaongeza kusema kua: “Kongamano la mwaka huu litatofautiana na ya miaka ya nyuma, kwani mwaka huu Iraq inasherehe za kukomboa ardhi yake dhidi ya magaidi wa Daesh, hivyo tunatarajia awamu hii iwe ya tofauti”.

Kumbuka kua hili ni miongoni mwa makongamano makubwa ya dini ambayo hufanywa kila mwaka kwa ajili ya kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s), linalenga kuonyesha nafasi ya Imamu (a.s), na kubainisha msimamo wake dhidi ya kiongozi wa zama zake ambaye ni Muawiya, sambamba ya kuangalia mitihani na matatizo aliyopata (a.s) katika uhai wake, pamoja na kutaja usia na hadithi za kimalezi na kiibada za Imamu (a.s), na kuangalia misingi ya ubinadamu aliyo kua nayo (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: