Atabatu Abbasiyya tukufu inatoa huduma za kibinadamu kwa taasisi ya Al-Fadhil ya kulea mayatima…

Sehemu ya huduma za matibabu zinazo tolewa na Atab
Miongoni mwa mambo yanayo tiliwa umuhimu mkubwa na Atabatu Abbasiyya tukufu ni swala la kulea mayatima, hususan mayatima wa mashahidi wa Fatwa ya kujilinda, ambapo hutoa huduma moja kwa moja kwa mayatima au kwa kutumia taasisi zinazo lea mayatima, miongoni mwa taasisi hizo ni Al-Fadhil ya kulea mayatima iliyopo katika mji wa Najafu na inalea makumi ya mayatima.

Mkuu wa taasisi hiyo Shekh Hussein Turabi ametuambia kazi zinazo fanywa na taasisi na huduma wanazo pewa na Atabatu Abbasiyya kua: “Tunapo ongelea mashahidi wa Hashdi Sha’abi na mayatima wao, hakika maneno hua na muelekeo mwingine, na mzungumzaji huhisi jukumu kubwa alilonalo la kuwaenzi watu amboa walijitolea kila walicho nacho kwa ajili ya kulinda dini, heshima na ardhi tukufu”.

Akaongeza kusema kua: “Taasisi ilianzishwa (1/3/2017m) na kusajiliwa kama taasisi isiyo kua ya serikali, inafanya kazi ya kutunza mayatima wa Iraq kwa ujumla hususan mayatima wa mashahidi, inawapa malezi bora yatakayo wafanya wawe watu wema katika jamii watakao changia ujenzi wa taifa, kama wazazi wao walivyo changia kulinda taifa kwa kutoa roho zao, taasisi inagharamia shughuli zake kutokana na msaada inao pata kutoka katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kwa wahisani wengine miongoni mwa waumini”.

Turabi akabainisha kua: “Taasisi inalenga kutoa huduma za kibinadamu na kijamii pamoja na chakula na mengineyo kwa mayatima wa Hashdi Sha’abi na familia zao, pamoja na kuwasaidia kuinua kiwango chao cha elimu, inalea na kutunza mayatima wa jinsia zote, wanaume hadi kufikia umri wa kubalehe na wasichana hadi watakapo olewa, pia inatoa misaada mbalimbali kwa mafakiri, miongoni mwa mambo yanayo fanywa na taasisi hii ni:

  • 1- Kugawa nafaka za chakula na mavazi kwa mayatima na familia zao kupitia vituo vya shirika la Nurul-Kafeel lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu vilivyo eneo mikoani, na hutenga kiwango maalumu cha pesa kila mwezi na kuzikabidhi kwa yatima kupitia shirika la Nurul-Kafeel au vituo vya biashara.
  • 2- Hupanga ziara za mayatima na familia zao kwenda kutembelea maeneo matukufu ya ndani na nje ya Iraq kwa kushirikiana na kitengo cha usafiri cha Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • 3- Kuchangia katika kutafuta kazi za kujikimu kimaisha kwa mayatima na familia zao, kama vile kushiriki katika kozi mbalimbali za ushonaji na upishi na zinginezo.
  • 4- Kufungua shule za awali, Maahadi na vituo vya viziwi na watu wenye ulemavu hususan mayatima wa Hashdi Sha’abi, kabla ya mwaka mmoja tulifungua shule ya awali ya mayatima ambayo wanasoma bure.
  • 5- Kugharamia matibabu ya wajane na mayatima wa Hashdi Sha’abi waliopo ndani na nje ya Iraq wenye hali mbaya, tumesha fanya makubaliano na hospitali ya rufaa Alkafeel ambayo ipo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu watoe matibabu bure kwa watu watatu kila mwezi hata kama matibabu hayo yatagharimu kiasi gani.
  • 6- Kuwajenga mayatima kisaikolojia kwa kuwapa nadwa na mawaidha mbalimbali ili kuwafanya wajiamini na wawe raia wema.
  • 7- Kufanya tafiti za kielimu pamoja na kufanya sensa ya familia za mafakiri na familia za mashahidi na mayatima kwa kushirikiana na taasisi za kielimu, sambamba na kuunda kamati katika miji yote kwa ajili ya kuwatambua mayatima na mafakiri na kusaidia kufikia malengo ya taasisi.
  • 8- Kuimarisha ushirikiano na taasisi za serikali na zisizo kua za serikali za ndani na nje ya Iraq kwa ajili ya kubadilishana uzowefu na kufanikisha malengo ya taasisi.
  • 9- Kuiwezesha taasisi ya kulea mayatima na familia zao kuweza kutekeleza majukumu yake kwa kutumia njia mbalimbali.

Unaweza kuwasiliana na taasisi kwa Email: alfadael.fondation@gmail.com au piga simu namba: (07718466503 au 07601608978).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: