Ofisi ya Marjaa dini mkuu Mheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani imetangaza kua kesho Alkhamisi (17 Mei 2018m) ni siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, hivyo:
Uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu unatoa pongezi kwa Imamu wa Zama (a.f) na Maraajii dini wakuu na kwa kila muislamu duniani kwa kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani, tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu akubali ibada zenu katika mwezi huu mtukufu na awawezeshe kufanya kila jambo la kheri hakika yeye ni msikivu na mjibuji..
Tunatoa pongezi maalumu kwa wale walio itikia wito wa Marjaa dini mkuu, majemedari wa Hashdi Sha’abi na wanajeshi wa serikali, walio pigana kuihami Iraq na raia wake pamoja na maeneo matukufu na bado wapo makambini kwa ajili ya kuimarisha usalama wa taifa hili, tunawaambia: Mwezi mtukufu wa Ramadhani umekuja enyi ambao Marjaa dini mkuu alisema kuhusu nyie: (Nyie ndio utukufu wetu na fahari yetu) (Enyi ambao hatuna wengine wa kujifaharishia zaidi yenu) (Mmekua na majukumu makubwa zaidi).
Pia tunatuma salamu za pongezi rasmi kwa familia za mashahidi na kwa majeruhi walio pandisha bendera ya uhuru kwa damu zao tukufu, wakaondoa giza lililo kua limewafunika Wairaq kwa muda wa miaka mitatu, hatimae wananchi wa Iraq leo hii watafanya Ibada za mwezi huu mtukufu kwa amani na utulivu.
Tunamuomba Mwenyezi Mungu mtukufu aurudishe tena mwezi huu kwa watu wote ukiwa na heri na baraka na awawezeshe kufanya kila jambo la kheri na lenye manufaa.