Mwenyezi Mungu mtukufu anasema: ((Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’an kua ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi na uongofu na upambanuzi)).
Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu amewawekea waja wake nyakati maalumu ambazo wanashindana katika kufanya mambo ya heri, na kukithirisha ibada pamoja na kujikurubisha kwake, kwa kufanya nyeradi na kuomba dua, miongoni mwa nyakati hizo tukufu ni mwezi wa Ramadhani, mwezi wa Qur’an, kheri, baraka, sadaka na Dua, hakika huu ni mwezi wa kuswali, ni mwezi wa kufanya mema, hakika ni mwezi wa kuachwa huru na moto kwa atakaye tubia kwa Mwenyezi Mungu mtukufu.
Enyi waumini: yatupasa tuutumie vizuri mwezi huu mtukufu, mgeni huyu ambaye anapo kuja kwetu huondoka haraka, tulikua tunasema kesho au baada ya kesho ni Ramadhani, baada ya siku chache tutasema: Umeisha mwezi wa Ramadhani, hivyo ndio siku za kheri zinavyo kuaga, siku za baraka na rehma huisha haraka, Allah Allah katika siku hizi, Allah Allah katika siku za Qur’an, Allah Allah katika mwezi wa funga, Allah Allah katika mwezi wa kisimamo… imepokewa katika khutuba ya Mtume (s.a.w.w) aliyo itoa kwa kuukaribisha mwezi wa Ramadhani, kama ilivyo ripotiwa na Huru Al-A’amili katika kitabu cha Wasaailu Shia (juzu 10/ uk 313) anasema: Hakika umekujieni Mwezi wa Mwenyezi Mungu na baraka, rehema na maghfirah, mwezi ambao ni mbora zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu kushinda miezi mingine, na siku zake ni bora kushinda siku zingine, na usiku wake ni bora kushinda usimu mwingine, na saa zake ni bora kushinda saa zingine, ni mwezi ambao mmeitwa katika ugeni wa Mwenyezi Mungu, na mmefanywa kua wakirimiwa wa Mwenyezi Mungu, pumzi zenu mnaandikiwa thawabu za tasbihi, usingizi wenu mnaandikiwa thawabu za kufanya ibada, ibada zenu zinakubaliwa, dua zenu zinajibiwa, muombeni Mwenyezi Mungu kwa nia safi, akuwezesheni kufunga na kusoma kitabu chake.
Hakika mwenye hasara zaidi ni yule atakaye kosa msamaha wa Mwenyezi Mungu katika mwezi huu, kumbukeni kwa njaa yenu na kiu chenu njaa ya siku ya kiyama na kiu chake, wapeni sadaka mafakiri na masikini wenu, waheshimuni wakubwa wenu na muwahurumie wadogo zenu, ungeni undugu wenu na hifadhini ndimi zenu, msiangalie mambo yasiyo faa kuangaliwa na macho yenu, wala msisikilize yasiyo faa kusikilizwa, wahurumieni mayatima wa watu, na watu watawahurumia mayatima wenu, fanyeni toba kwa Mwenyezi Mungu akusameheni madhambi yenu, inuweni mikono wakati wa kuomba kwenu dua…).