Ramadhani katika kumbukumbu ya Karbala: Siku ya kwanza ya kuandama kwa mwezi mtukufu moja ya alama za kiimani baina ya watu wa Karbala na Marjaa dini mkuu…

Maoni katika picha
Hakika kuuona muandamo wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ni jambo kubwa sana linalo fungamana na utukufu wa Qur’an, watu wa Karbala mwishoni mwa mwezi wa Shabani wote huelekeza macho yao sehemu linapo tua jua wakiangalia kuandama kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani, utawakuta wanaume wamesimama kila kona wakiangalia kuandama kwa mwezi, na wengine wamepanda juu ya paa za nyumba zao ili wauone kwa urahisi, na wasipo uona utawakuta wanaelekea katikati ya Karbala na Najafu wakisubiri kwa hamu taarifa za mwezi.

Ustadhi Ali Khabbaaz anatuhadithia mazingira aliyo shuhudia ya kuandama kwa mwezi wa Ramadhani katika miongo aliyo ishi kua: “Hakika kipindi cha kuandama mwezi wa Ramadhani kina siri zake kwa watu wa Karbala, kuna harakati fulani hufanywa na wanaume katika kutafuta mwezi mwandamo, jambo hilo walikua wanalipa umuhimu mkubwa sana, walikua wanatuma ujumbe wa watu kwenda katika mji wa Najafu kutafuta taarifa za kuandama kwa mwezi, kwani kipindi hicho hawakua na njia nyingine wanayo tegemea kutapa taarifa kama vile redio, nakumbuka watu wa Karbala walikua wanajaa njiani wakisubiri watu walio tumwa Najafu warudi, kwani ni watu hao tu ndio waliokua wanakuja na habari za kuaminika, kulikua na uhusiano mkubwa sana baina ya Maraajii dini na watu wa Karbala, hakika Karbala haijawahi kujitenga na Maraajii hata wakati mmoja”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: