Atabatu Abbasiyya yaanza ratiba yake ya usomaji wa Qur’an katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ndani ya ukumbi wa haram tukufu…

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya kupitia Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu imeanza kutekeleza ratiba ya usomaji wa Qur’an ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, katika mazingira bora yenye utulivu mkubwa karibu na malalo ya Abulfadhil Abbasi (a.s), zimesikika sauti za usomaji wa kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kushiriki kundi kubwa la waumini na mazuwaru watukufu.

Usomaji wa Qur’an Tartiil ni miongoni mwa ratiba muhimu za Atabatu Abbasiyya tukufu katika mwezi wa Ramadhani, maandalizi ya kisomo hiki yalifanyika mapema kwa kuandaa jukwaa pamoja na sehemu za kukaa washiriki wa usomaji sambamba na kuandaa idadi kubwa ya misahafu.

Shekh Jawadi Nasrawi mkuu wa Maahdi ya Qur’an tukufu amezungumza kuhusu ratiba hii kua: “Usomaji wa Qur’an Tartiil ni moja ya harakati muhimu za Maahadi katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, mwezi ambao sio sawa na miezi mingine na michana yake ni bora kuliko michana ya miezi mingine yote, na usiku wake ni bora kuliko usiku mwingine wowote, hivyo ataba tukufu huupa umuhimu maalumu wa kusoma Qur’an katika mwezi huu kila mwaka, hakika mwezi huu unauhusiano wapekee na Qur’an tukufu, kwani usomoja wa Qur’an unasaidia kukomaza roho kiibada”.

Akaongeza kusema kua: “Kisomo cha Qur’an kila siku kitaanza saa kumi na moja jioni na litasomwa juzuu kamili, imeandaliwa sehemu maalumu ndani ya ukumbi mtukufu wa haram na imepangwa misahafu kwa ajili ya kutoa nafasi ya kushiriki watu wengi, na vipaza sauti vimeandaliwa vizuri zaidi, pamoja na jukwaa zuru, usomaji ni wa mmoja mmoja ambapo kuna wasomaji watano husoma kwa kupokezana na wengine wanafuatilia kisomo kwa sauti za chini, jumla ya muda wanao tumia kusoma ni saa moja, ratiba hii itaendelea kila siku hadi mwisho wa mwezi, kisomo hiki kinarushwa moja kwa moja katika vyombo vya habari (Chanel ya Qur’an tukufu, Furaat, Imamu Hussein, Anwaar na Mahdi) kumbuka kua upigaji wa picha unafanywa na watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu idara ya picha na uzalishaji ya kitengo cha habari na utamaduni chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu”.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya imesha andaa ratiba maalumu ya kuhuisha siku za mwezi huu mtukufu kwa kusoma Qur’an na kufanya mashindano ya Qur’an, sawa iwe katika Maahadi au katika matawi yake yaliyo enea katika mikoa mbalimbali ya Iraq, kwa ajili ya kusambaza utamaduni wa Qur’an katika mwezi huu mtukufu, na kusaidia kuisoma Qur’an nzima katika mwezi huu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: