Kuhitimisha ushiriki wake kwa kupiga kura ya shindano la kitamaduni: Atabatu Abbasiyya tukufu yakamilisha kwa mafanikio ushiriki wake katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa awamu ya (31) mjini Tehran…

Maoni katika picha
Kwa muda wa siku 12, na kwa kazi tofauti za tawi lake, mwishoni mwa mwezi wa Shabani wa mwaka 1439h, Atabatu Abbasiyya tukufu imehitimisha ushiriki wake katika maonyesho ya vitabu ya kimataifa awamu ya thelathini na moja.

Haya yameelezwa na Ustadh Jasaam Muhammad Saidi kiongozi wa kitengo cha machapisho kilicho shiriki katika maonyesho hayo, amesema kua: “Machapisho ya Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya yalikua zaidi ya aina 750, pia kulikua na shindano la kitamaduni na harakati zingine sambamba na ziara kwa niaba, na vikao vya kujadiliana pamoja na ziara za wageni”.

Akaongeza kusema kua: “Mwishoni mwa maonyesho ilipigwa kura kati ya majibu sahihi ya shindano la kitamaduni lililo endeshwa na tawi hili”.

Akafafanua kua: “Tumegawa aina mbili za zawadi, aina ya kwanza ni pete za fedha zilizo tengenezwa na Ataba mbili tukufu na kupambwa na kipande cha marumaru kilicho fanyiwa tabaruku katika Ataba hizo, pete (10) zimetoka katika Atabatu Husseiniyya tukufu, kila moja ina kipande cha marumaru kutoka katika kaburi tukufu, na Atabatu Abbasiyya tukufu pete (70) ambazo pia zina kipande cha marumaru kutoka katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), na vipande (80) vya marumaru vilivyo wekwa katika kitambaa kilicho fanyiwa tabaruku katika kaburi tukufu”.

Akabainisha kua: “Zawadi zimegawiwa kwa kupiga kura ya wazi ambayo makumi ya watu wameshiriki”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: