Dokta Salmaan Haadi Aali Twa’amah anatuhadithia siku za mwezi wa Ramadhani katika mji wa Karbala, anasema: Hakika mwezi huu mtukufu katika mji wa Karbala unatofautiana na miezi mingine, kuna mambo ambayo hufanyika na pengine huwezi kuyakuta yakifanyika katika miji mingine ya Iraq, kuna watu wanafanya ibada mfululizo, wanasoma Qur’an tukufu na dua mchana na usiku, kwa kiwango cha chini husoma juzuu moja kila siku, hadi ikifika siku ya Idi wanakua wamemaliza Qur’an nzima, hivyo wanakua wamejivunia thawabu nyingi, au wakati mwingine wanahudhuria vikao vya kusoma Qur’an tajwidi katika nyakati za usiku.
Na kundi lingine hushindwa kufunga kwa sababu za maradhi au safari, kama inavyo sema Qur’an tukufu: (Na atakaye kuwa miongoni mwenu mgonjwa au yumo safarini basi atimize hesabu katika siku nyengine) surat Baqarah aya ya 184.
Katika mji mtukufu wa Karbala, vilikua vinafanyika vikao vya kielimu ambavyo ni sawa na shule, wanachuoni na watu watukufu walikua wanafanya vikao hivyo kila siku, wakizungumza mazingira halisi ya kijamii na mambo ya ubunifu na yenye manufaa, na washairi wakisoma mashairi murua yenye ujumbe wa matukio mbalimbali, huku vituo vya kidini vikiadhimisha kila tukio, hivyo tunaona malezi ya watu wa Karbala yameweza kuathiri muonekano wa nje, kutokana na mazingira imara ya kidini walio nayo.
Kuna vikao vya kuomboleza ambavyo hufanywa katika kumbi tukufu za haram mbili, au katika misikiti na masokoni, na katika viwanja vya umma na ndani ya nyumba za watu, alikua anapanda mimbari Sayyid Jawaad Hindi, na kuanza kuelezea kwa kiasi alicho jaliwa kutokana na mazingira ya tukio husika, kisha wanafuata makhatibu wengine kama vile Sayyid Hassan Istirabadi, na Shekh Muhammad Hassan na mwanaye Shekh Muhsin Abul Hubbi na Shekh Haadi Khafaaji na Shekh Abduzaharaa Ka’abi, na Sayyid Murtadha Kazwini na Sayyid Swadri Dini Alhakim Shahristani na wengineo…
Mwenyezi Mungu mtukufu ameujalia mwezi huu kua mwezi wa baraka, rahma na ridhaa yake tofauti na miezi mingine, kama ilivyo michana yake usiku wake na saa zake ni bora kuliko zingine zote, kama alivyo sema Mtume Muhammad (s.a.w.w) katika khutuba aliyo toa Ijumaa ya mwisho ya mwezi wa Shabani: (Enyi watu.. Hakika umekujieni mwezi wa Mwenyezi Mungu na baraka, rehma na maghfirah, mwezi bora mbele ya Mwenyezi Mungu kushinda miezi yote, na siku zake ni bora kushinda siku zote na saa zake ni bora kushinda saa zote…hadi mwisho).
Na siku muhimu zaidi katika mwezi huu ni mwezi kumi na tano, kwa sababu ni tarehe aliyo zaliwa mjukuu mkubwa wa Mtume Imamu Hassan Almujtaba (a.s), aliye tuonyesha njia ya utukufu, na akatuangazia njia sahihi ya maisha.