Maahadi ya Qur’an tukufu yafanya awamu ya nne ya mashindano ya Qur’an ya vikundi.

Maoni katika picha
Kutokana na muendelezo wa awamu tatu zilizo pita na kuonyesha mafanikio makubwa, jioni ya jana siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ilianza awamu ya nne ya mashindano ya Qur’an tukufu ya vikundi, yanayo simamiwa na kituo cha kuandaa wasomi na mahafidhi wa Qur’an chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu ya Atabatu Abbasiyya, na kwa ushiriki wa vikundi mbalimbali vya Qur’an kutoka mikoa ya Iraq, mashindano yataendelea kwa muda wa siku (15) kila siku vitashiriki vikundi vinne kwa kuulizwa maswali tofauti, mashindano yalianza kwa kushindanishwa kikundi cha mkoa wa Waasit na Karbala (B) na hatua ya pili ilikua baina ya kikundi cha Bagdadi na Karbala (A).

Mashindano haya kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi wa kituo cha kuandaa wasomi na mahafidhi wa Qur’an Sayyid Hasanaini Halo: “Ni sehemu ya ratiba ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya mwezi wa Ramadhani iliyo andaliwa kwa ajili ya kuhuisha siku za mwezi huu mtukufu, mashindano haya yanahusu vipengele tofauti vya Qur’an, na washiriki wanatoka mikoa mbalimbali ya Iraq, kila kikundi kinakua na watu watatu (Msomaji, Haafidh na Mfasiri) na wanaulizwa maswali ya aina tatu, kusoma, kuhifadhi na tafsiri”.

Akaongeza kusema kua: “Maswali yanaulizwa kwa njia tofauti, kuna maswali anayapata kwa kutumia kura, anachukua aya ambazo zinatakiwa zisomwe kwa mahadhi fulani, na msomaji analazimika kuzisoma kwa mahadhi hayo, au inafunguliwa sauti ya mmoja wa wasomi wa zamani halafu anaulizwa msomaji ataje jina la msomi huyo, kuhusu kipengele cha kutafsiri, anaulizwa maana ya aya na kuna maswali mengine yanahusu sheria za Qur’an, na haafidhi anaulizwa kuhusu hifdhu, kwa mfano anaambiwa kamilisha aya fulani, au kisomo cha kufukuzana baina ya mahafidhi wawili, hafidhi wa kwanza anasoma aya fulani na hafidhi mwingine anaendelea pale alipo ishia mwenzake, kisomo hicho huitwa kisomo cha kufukuzana katika hifidhu”.

Akaongeza kua: “Kuna kamati ya majaji inaundwa na watu wanne, ambao wanaangalia hukumu za usomaji, sauti, naghma, tafsiri, mada, kusimama, kuanza na hifdhu, pia kuna maswali wanayo ulizwa mazuwaru, na kila siku mwana familia mmoja wa shahidi wa fatwa ya kujilinda anapewa zawadi”.

Kumbuka kua mashindano haya ni sehemu ya harakati maalumu za Qur’an zinazo simamiwa na Maahadi ya Qur’an katika mwezi huu mtukufu, na wanashiriki watu kutoka mikoa tofauti ya Iraq, shindano hili linahusisha, hukumu za usomaji, hifdhu na tafsiri, na yanarushwa na vyombo mbalimbali vya habari kupitia masafa maalumu ya bure iliyo andaliwa na kituo cha uzalishaji Alkafeel.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: