Wakati wowote ukiingia katika mji wa Karbala utawakuta watu wanaulizana, (Lini unaisha mwezi wa Shabani? Hivi mwezi huu unasiku thelathini au ishirini na tisa? Nani atakaye tumwa kwenda Najafu kwa ajili ya kupata uhakika wa taarifa za mwezi?....) kila mtu utamkuta anazungumza habari hizo, iwe ndani ya nyumba, kwa watengeneza mikate, buchani na sehemu zingine, wanawake kwa wanaume wazee kwa watoto, hiyo ndio Karbala watu wake huwa na shauku kubwa sana ya kufanya ibada ya funga, kuswali na kusoma dua.
Unapo karibia kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani utaona nyuso za watu wa Karbala zilivyo jaa tabasamu, na utaona namna watu wanavyo jiandaa kuupokea, utaona kilele cha furaha yao pale mwezi utakapo onekana, au watakapo rudi na taarifa ya kuonekana mwezi wajumbe walio tumwa Najafu.
Ustadh Ali Khabaaz kiongozi wa idara ya habari ya Atabatu Abbasiyya tukufu ametuhadithia kua: “Kwa uwazi kabisa inaonyesha mwezi huu mtukufu katika mji wa Karbala unatofautiana na miezi mingine, kuna mambo yanayo fanyika katika mji huu ambayo huwezi kuyaona katika miji mingine ya Iraq, Karbala ya zamani ilikua na mambo yake, baadhi ya mambo ya zamani tuliyaona tena baada ya mwaka 2003m, watu wa Karbala walikua na kawaida mwezi wa Ramadhani unapo ingia wanahudhuria katika majlisi mwezi mzima, majlisi hizo zilikua zikifanywa katika haram ya Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), pamoja na katika baadhi ya vyuo na Husseiniyya zilizopo kila kona ya mji wa Karbala, hivyo watu wa Karbala walikua hawakosekani katika majlisi hizo kila siku ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani”.