Idara ya makhatibu wa kike yafanya vikao vya usomaji wa Qur’an ndani ya mwezi wa Ramadhani kila siku asubuhi…

Sehemu ya kikao cha usomaji wa Qur’an
Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa Qur’an, ni mwezi mtukufu ambao Mwenyezi Mungu ameteremsha ndani yake Qur’an kitabu chenye kubainisha kila kitu, na umefanywa kua mwezi bora kushinda miezi yote, michana yake ni bora kushinda michana inayo patikana katika miezi yote na usiku wake ni pora kuliko usiku zingine zote na saa zake ni bora kuliko saa zote, mwezi huu ndio ambao Mwenyezi Mungu amejaalia siku ya Lailatul Qadri ambayo ni siku bora zaidi ya miezi elfu moja, kwa ajili ya kunufaika na mwezi huu mtukufu, idara ya makhatibu wa kike ya Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa ratiba maalumu kwa ajili ya mwezi huu, ikihusisha vikao vya kusoma Qur’an kila siku asubuhi.

Vikao hivi kila siku asubuhi hufanyika katika Sardabu (ukumbi wa chini) wa Imamu Mussa Alkadhim (a.s), katika eneo lililo panuliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu, vikao hivyo vinafanyika kila siku, chini ya ushiriki wa wanafunzi na mazuwaru watukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), vikao hivi huanza saa nne hadi saa sita asubuhi, miongoni mwa ratiba yake ni:

  • 1- Kusoma juzuu moja la Qur’an tukufu.
  • 2- Kufafanua maana za maneno yaliyo patikana katika juzuu iliyo somwa na kusherehesha baadhi ya mafundisho yake.
  • 3- Kuuliza swali kuhusu hadithi za kiimani zinazo himiza tabia njema za kiislamu kutoka kwa Mtume na Ahlulbait (a.s), zenye uhusiano na aya zilizo somwa katika juzuu husika.
  • 4- Kusoma (kisa au mazingatio) yanayo fafanua baadhi ya matukio ya kihistoria yaliyo tokea katika siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani na baadhi ya visa vya Qur’an tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: