Mwezi wa Ramadhani vimeshushwa ndani yake vitabu vya Mwenyezi Mungu…

Maoni katika picha
Amesema Mwenyezi Mungu mtukufu: (Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur’an kuwa ni uongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi na uongofu na upambanuzi), na Mtume (s.a.w.w) anasema katika khutuba ya kuupokea mwezi wa Ramadhani kua: (Enyi watu… Hakika umekujieni mwezi wa Mwenyezi Mungu na baraka, rahma na maghfirah, mwezi mbora kuliko miezi yote, na siku zake ni bora kuliko siku zote, na usiku wake ni bora kuliko usiku wowote, na saa zake ni bora kuliko saa zote).

Mtume alibainisha kua Mwenyezi Mungu aliutukuza mwezi wa Ramadhani kwa kuteremsha vitabu vyake vitano ndani ya mwezi huo, katika mwezi huu Mwenyezi Mungu mtukufu aliteremsha nyaraka za Mtume Ibrahim (a.s) na Taurati kwa Nabii Mussa (a.s), na Injili kwa Nabii Issa (a.s), na Zaburi kwa Nabii Daudi (a.s).

Imepokewa kutoka kwa Imamu Jafari bun Muhammad Swadiq (a.s) anasema: “Qur’an ilishushwa mara moja katika mwezi wa Ramadhani hadi katika Baitul-Ma’amur, kisha ikateremka kidogo kidogo ndani ya miaka ishirini, kisha Mtume (s.a.w.w) akasema: Nyaraka za Ibrahim ziliteremshwa siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, na Taurati iliteremshwa siku ya sita ya mwezi wa Ramadhani, na Injili ikateremswa siku ya kumi na tatu ya mwezi huo, na Zaburi siku ya kumi na nane, na ikateremshwa Qur’an siku ya ishirini na tatu ya mwezi huu wa Ramadhani”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: