Miongoni mwa huduma zinazo tolewa na Atabatu Abbasiyya kwa wakazi wa mitaa hiyo ni:
- 1- Kurahisisha uingiaji wa wakazi katika eneo hili kwa kuweka mtu maalimu katika kila kituo cha ukaguzi.
- 2- Kurahisisha kuingiza vifaa wanavyo hitaji wakazi ambavyo kwa kawaida hua vinahitaji kibali kutoka kwa maafisa usalama ndio viingie katika eneo hili.
- 3- Kukarabati barabara na mitaa na kuiwekea umeme.
- 4- Kupanda miti katika mji wa zamani, inayo changia kupendezesha mji na kuboresha mazingira.
- 5- Katika vituo vya (RO) vinavyo gawa maji, mkazi anaruhusiwa kuchukua kiasi chochote cha maji anayo hitaji.
- 6- Kuzibua mitaro pale inapo ziba kutokana na maji ya mvua au kwa sababu nyingine yeyote.
- 7- Hupewa huduma za matibabu kwa haraka kupitia vituo vya afya vya Ataba tukufu, sambamba na huduma ya gari ya kubeba wagonjwa kwa ajili ya kumpeleka hospitali za karibu wakati wowote inapo hitajika.
- 8- Kupangilia utembeaji wa mazuwaru kwa ajili ya kupunguza msongamano katika njia za pembeni ya haram tukufu zinazo pita madukani.
- 9- Kusaidia kuimarisha ulinzi, kwani usalama wa mitaa hiyo ndio usalama wa Ataba tukufu.