Maahadi ya Qur’an tukufu kitengo cha wanawake katika Atabatu Abbasiyya tukufu yaendesha ratiba ya Qur’an katika mwezi wa Ramadhani…

Maoni katika picha
Mtume (s.a.w.w) anasema: (Hawata kusanyika watu katika nyumba miongoni mwa nyumba za Mwenyezi Mungu wakisoma kitabu cha Mwenyezi Mungu na wakifundishana, ispokua watateremshiwa utulivu na watafunikwa na rehma na kupepewa na malaika na Mwenyezi Mungu atawakumbuka kwa kitendo chao hicho), unapo kuja mwezi wa Mwenyezi Mungu na baraka, rehma na maghfira, mwezi huu ambao ni mbora kushinda miezi yote, na siku zake ni bora kuliko siku zote, na usiku wake ni mbora kuliko usiku wote, na saa zake ni bora kuliko saa zote, mwezi ambao waislamu wameitwa katika ugeni wa Mwenyezi Mungu, na yeye ndiye anaye wakirimu, kwa ajili ya kunufaika na mazingira haya ya kiroho na kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu mtukufu, Maahadi ya Qur’an tukufu tawi la wanawake chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu imeandaa ratiba ya usomaji wa Qur’an kwa wanawake katika makao makuu ya Maahadi iliyopo Najafu na katika matiwi yake yaliyopo mikoani.

Ratiba ya usomaji wa Qur’an ni sehemu ya ratiba kuu iliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kuhuisha siku za mwezi huu mtukufu, na usomaji wa Qur’an umepewa umuhimu mkubwa, sawa iwe kwa wanaume au wanawake.

Miongoni mwa vipengele vya ratiba hii ambayo inatofautiana baina ya kitengo na kitengo kingine, lakini inafanana katika maudhui kuu, ambayo inahusu usomaji wa Qur’an na Dua Iftitaahi pamoja na dua zingine, sambamba na kufafanua vipengele muhimu katika aya zinazo somwa, pamoja na mashindano madogo madogo.

Kumbuka kua ratiba hii itaendelea hadi mwisho wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, Maahadi inalenga kunufaika na mwezi wa Ramadhani kwa kuimarisha uhusiano baina ya Qur’an tukufu na wakina mama, na kuwahimiza umuhimu wa kujifunza usomaji sahihi wa Qur’an tukufu na elimu zingine, pamoja na kusambaza utamaduni wa Qur’an na kuwafahamisha umuhimu wa kusoma Qur’an katika kikundi.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: