Ramadhani katika kumbukumbu ya Karbala: Daku…

Maoni katika picha
Inawezekana mwili ukawa tayali kupoteza moja ya kiungo chake kwa ajili ya kuhifadhi milango yake ya fahamu, kwa sababu milango ya fahamu ndio hutoa ladha ya maisha hapa duniani, unapo poteza mlango mmoja wa fahamu hua ni hasara kubwa sana, na hiyo ndio hali ya mataifa kihistoria, ambapo hua kuna mambo wanayo fungamana nayo kijamii na kufungamanisha kizazi na kizazi kingine, usiku wa mwezi wa Ramadhani barabara hujaa waamsha daku, utakuta watu wakizunguka usiku kucha wakipiga ngoma huku wanasema amkeni mle daku, wakati wa daku umefika, ikiwa ni kawaida ya kuwaamsha watu wale daku.

Kiongozi wa idara ya habari wa Atabatu Abbasiyya tukufu Ustadh Ali Khabaaz ametuhadithia mazingira ya uamshaji wa daku yaliyo baki katika akili za watu wa Karbala kwa miaka mingi, mazingira ambayo bado yanaendelea hadi sasa bamoja na maendeleo ya teknolojia ya sasa.. na maendeleo ya vyombo vya mawasiliano.

Khabaaz amesema kua: “Watu wa Karbala baada ya kurudi majumbani kwao usiku na kutoka katika haram tukufu, na kutawala ukimwa katika mitaa na nyumba za watu, na baadhi ya watu kulala usingizi, husikika sauti ya muamsha daku (Ashuur asiye ona) wengine wanamwita (Abuu Twabal) aliye kua muamshaji maarufu wa daku, yeye pamoja na watu walio ungana naye katika kazi hiyo, Ashuur alikua na staili maalumu ya uamshaji wa daku, miongoni mwa mambo ninayo kumbuka, ilikua mtu akipitiwa na usingizi, ikifika asubuhi anauliza; hivi jana Ashuur alipita? Hakika alikua kipenzi wa watu na alikua anapita kila nyumba bila kuchagua. Inapo fika siku ya Idi Ashuur alikua anapita asubuhi akiwa pamoja na kundi la watoto anatoa pongezi kwa kufika siku ya sikukuu kwa wale aliokua anawaamsha usiku kwa ajili ya kula daku ndani ya mwezi wa Ramadhani, alikua hana kiwango maalumu cha malipo, kila mtu alimpa kiasi alicho jisikia kama zawadi ya sikukuu”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: