Usomaji wa Qur’an tukufu ni dhikri bora zaidi mbele ya Mwenyezi Mungu mtukufu, ni ibada tukufu mno, kuna thawabu nyingi ambazo hazielezeki, hiyo ni katika miezi ya kawaida, unapo ingia mwezi wa Ramadhani utukufu huongezeka mara dufu, hakika mwezi wa Ramadhani huitwa mwezi wa Qur’an, bali ni msimu wa Qur’an, kila kitu kina msimu na msimu wa Qur’an ni mwezi wa Ramadhani.
Usomaji wa Qur’an Tartiil ni moja ya vipengele muhimu sana katika ratiba ya Maahadi ya Qur’an ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mwezi huu wa Ramadhani, na inasomwa kila siku katika haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kila siku husomwa juzuu moja, kisomo hicho huhudhuriwa na watu wengi sana na huongozwa na wasomaji wa kimataifa.
Kamera ya mtandao wa Alkafeel inakuletea picha za vikao vya usomaji wa Qur’an tukufu vinavyo fanyika kila siku jioni ndani ya haram tukufu ya Abulfadhil Abbasi (a.s).