Kumbukumbu ya kihistoria: Mwezi sita Ramadhani ilikua siku ya Wilayatul Ahdi ya Imamu Ridhaa (a.s)…

Maoni katika picha
Katika siku kama ya leo, mwezi sita Ramadhani mwaka (201h) kilitangazwa kiapo cha utii (baiyya) kwa Imamu Ridhaa (a.s) cha Wilayatul Ahdi kilicho shurutishwa na Ma-Amun kiongozi wa bani Abbasi, kipindi hicho kilikua muhimu sana katika historia ya maisha yake (a.s), baada ya miaka miwili tangu kushika madaraka kwa Ma-Amun alianza kumwita Imamu Ridhaa kwenye uongozi, alimuandikia barua nyingi za kumtaka akubali madaraka, lakini Imamu alikua anakataa, na wala hakuonyesha dalili ya kukubali madaraka hayo, hadi Ma-Amun akafikia kumtishia kifo, walifanya majadiliano mfululizo kwa muda wa miezi miwili.

Ma-Amun alikua na malengo tofauti ya kumpa uongozi wa ahadi (Wilayatul Ahdi) Imamu (a.s), miongoni mwa malengo yake ilikua ni kujaribu kutuliza hali ya wasiwasi iliyo kua imeenea kipindi hicho, na kujaribu kumdhibiti Imamu Ridhaa (a.s) na kumuweka mbali na wafuasi wake waliopo katika mji wa Madina na Iraq, na kudhoofisha upinzani.

Kutoka kwa Rayaan bun Swalat anasema: (Niliingia kwa Ali bun Mussa Ridhaa (a.s), nikamwambia: Ewe mtoto wa Mtume, hakika watu wanasema: umekubali uongozi wa ahadi (Wilayatul Ahdi) pamoja na zuhudi yako ya kuipa nyongo dunia!). Akasema (a.s): “Mwenyezi Mungu anajua namna nilivyo karahishwa katika jambo hili, nilipo hiyarishwa baina ya kukubali jambo hili au niuawe, nikaamua kukubali badala ya kuuawa, hivi watu hawajui kua Yusufu (a.s) alikua ni Mtume wa Mwenyezi Mungu, alipo ona kuna dharura ya kuchukua uongozi alisema: Niwekeni katika uongozi wa hazina hakika mimi ni muaminifu na mjuzi, na mimi nimelazimika kukubali ahadi ya uongozi baada ya kuhiyarishwa kukubali ahadi ya uongozi au kifo, mimi sikukubali jambo hili ispokua baada ya kulazimishwa, na Mwenyezi Mungu anajua na yeye ndiye tegemeo langu”.

Imamu (a.s) alikubali uongozi wa ahadi kwa masharti, na ilikua baada ya kutishiwa kifo, miongoni mwa masharti aliyo toa ni kwamba, hata toa amri wala hata kataza jambo wala kutoa hukumu au kubadilisha jambo lolote, hakika Imamu (a.s), hadi anafikia kuuawa kwa kupewa sumu hakushiriki katika mambo ya utawala ispokua kwa kiasi kidogo sana katika mambo ya kijamii.

Pamoja na hivyo Imamu (a.s) alifanikiwa kutibua njama za Ma-Amun dhidi yake, alikua na kundi kubwa la waumini walio kua wanamkubali na alikua akieleza maovu ya utawala wa bini Abbasi katika maeneo mengi, pia Imamu (a.s) alifanikiwa kuhuisha sunna za babu yake (s.a.w.w) na baba zake watukufu (a.s), ndipo Ma-Amun akamtaka aondoke Madina na aende Khurasani –katika makao makuu ya utawala wake- , Imamu (a.s) akakubali kwa shingo upande, Ma-Amun alidhani kua kutoka kwa Imamu katika mji wa Madina kutamjenga kisiasa na kutaonyesha wazi namna Imamu anavyo ukubali utawala wake, jambo hilo litamsaidia kuungwa mkono na watu wote wa Alawiyya na Abbasiyya na kudhofisha wapinzani wake. Katika siku kama ya leo Ma-Amun alifanya kikao kikubwa akatengeneza jukwaa mbili kubwa akakaa yeye na Imamu, na akamuamrisha mwanaye aanze kumpa baiyya (kura ya utii) Imamu (a.s), kisha akaamuru watu watowe kiapo cha utii kwa Imamu, na baada ya hapo akampa zawadi ya thamani, na akagawa midani ya dhahabu kwa wahudhuriaji, na washairi na makhatibu kwa kusoma mashairi na kutoa khutuba za kusifu tukio hilo, akaamuru jina la Imamu Ali litajwe misikitini, na zitengenezwe hela zitakazo kua na jina lake pamoja na laqabu yake, katika mwaka huo ndio jina la Imamu Ridhaa (a.s) lilitajwa katika mimbari ya Mtume (s.a.w.w) katika mji wa Madina na akaombewa dua.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: