Mashindano ya Qur’an ya vikundi yamaliza mzunguko wa pili kwa kusoma vikundi nane…

Maoni katika picha
Juma nne ya jana jioni ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ilikamilika hatua ya kwanza ya mashindano ya Qur’an tukufu ya vikundi na kitaifa sehemu ya nne, yaliyo andaliwa na kusimamiwa na kituo cha kuandaa wasomaji na mahafidh wa Qur’an tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu.

Katika hatua hiii kulikua na ushindani mkubwa sana baina ya vikundi washiriki, na matokeo yao yalikaribiana sana, jumla ya vikundi nane vimesoma ambavyo ni: (Nainawa na Bagdad vikundi viwili vya A na B, Diwaniyya, Waasit, Hashdi Sha’abi, Najafu na Dhiqaar), kutoka katika vikundi (16) vinavyo toka mikoa tofauti, vikundi hivi vitaingia katika mvunguko wa pili ili vipatikane vikundi vinne, na wataendelea kuchujwa hadi hatua ya fainali itakayo fanyika usiku wa kumi na tano wa mwezi mtukufu wa Ramadhani ikiwa kama sehemu ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s).

Kumbuka kua mashindano haya yana mizunguko (4) na vikundi washiriki vipo zaidi ya (16) kutoka katika mikoa tofauti, kila kikundi kina (msomaji, mfasiri na haafidh), mashindano yaha yanaendeshwa chini ya kamati ya majaji walio bobea katika fani za Qur’an, hao ndio wanao husika na kuuliza maswali kwa kufuata utaratibu ulio pangwa na ndio watakao tangaza matokeo, mashindano yanafanyika siku (15) mfululizo jioni.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: