Kufuatia kuingia kwa mwezi mtukufu wa Ramadhani: Nakala zote za msahafu uliochapishwa na Atabatu Abbasiyya zimeisha na kazi ya kuchapisha nakala mpya inaendelea…

Maoni katika picha
Msahafu ulio andikwa na kuchapishwa na Atabatu Abbasiyya tukufu –kupitia kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu- umekubalika sana ukilinganisha na misahafu mingine, maombi yameongezeka sana hususan ulipo karibia mwezi wa Qur’an, mwezi mtukufu wa Ramadhani, jambo lililo pelekea kumalizika kwa nakala zote za msahafu huo, ukizingatia kua ndio mfahafu wa kwanza kuandikwa na mikono ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuchapishwa katika kiwanda cha Alkafeel tena kwa ubora wa juu kabila, chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, hii pia ni miongoni mwa sababu zinazo fanya watu wavutiwe zaidi na msahafu huu.

Mkuu wa kitengo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha ambao ndio watekelezaji wa mradi huu, Shekh Dhiyaau Dini Zubaidi amesema kua: “Msahafu uliochapishwa na Atabatu Abbasiyya unasifa nyingi zinazo sababisha upendwe na wasomaji na kuchukuliwa kwa wingi katika maonyesho ya vitabu yanayo fanywa na Ataba tukufu, jambo hilo limetufanya tuchapishe idadi kubwa zaidi, tangu kutolewa kwa misahafu hii maombi yanaongezeka kila siku kutoka ndani na nje ya Iraq, hususan katika usiku wa Ijumaa ambao hushuhudia ongezeko la mazuwaru, na maombi yaliongezeka zaidi ulipo karibia mwezi mtukufu wa Ramadhani”.

Akabainisha kua: “Sasa hivi tunachapisha toleo la tano la msahafu huu, matoleo manne ya kwanza kila toleo lilikua na idadi tofauti, jumla tumesha chapisha nakala elfu ishirini na tano (25,000)”.

Fahamu kua msahafu huu unasifa nyingi, ukizingatia kua hakuna taasisi yeyote iliyo kua imesha wahi kuandika na kuchapisha msahafu hapa Iraq kama ilivyo fanya Atabatu Abbasiyya tukufu, miongoni mwa sifa za msahafu huu ni:

  • 1- Msahafu umeandikwa na Hamidi Sa’adi muandishi maarufu wa kiiraq, chini ya watalamu wa Atabatu Abbasiyya tukufu na nakshi za kiiraq kwa namna ambayo umekua msahafu halisi wa kiiraq Abbasiyya.
  • 2- Kituo kilizingatia kukusanya maneno yenye maana moja katika mstari mmoja, jambo hili limeongeza uzuri wa mpangilio wa maneno matakatifu.
  • 3- Tulizingatia kuweka idadi za kurasa za msahafu mtukufu sawasawa na idadi ya kurasa katika misahafu mingine iliyopo.
  • 4- Surat Fat-ha imepangiliwa vizuri kufuatana na maana ya maneno yake, kila mstari inamaana maalumu hususan mambo yanayo fungamana na aya ya mwisho.
  • 5- Katika kusanifu na kutengeneza gamba la nje umezingatiwa uzuri wa muonekano, limewekwa nakshi zinazo fanana na nakshi zilizopo katika kaburi la Abulfadhil Abbasi (a.s) pamoja na nenbo maalumu ya Atabatu Abbasiyya tukufu.
  • 6- Msahafu umeandikwa kwa hati ya (Naskhi) yenye muonekano mzuri na inasomeka kwa urahisi bila tabu.
  • 7- Msahafu huu unafanana sana na misahafu inayo tumika katika nchi za jirani, kuanzia alama za kusimama na vitu vingine.
  • 8- Umeandikwa kwa umaridadi na utalamu mkubwa na zimepangiliwa vizuri sura na aya zake pamoja na kurasa zake sambamba na uwekaji maridhawa wa nakshi na alama mbalimbali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: