Daraja za swaumu kwa mujibu wa wanachuoni wa Akhlaq…

Maoni katika picha
Imepokewa kutoka kwa Imamu Ali (a.s) anasema: (Hakika kufunga kwa moyo ni bora kuliko kufunga kwa ulimi, na kufunga ulimi ni bora kuliko kufunga tumbo) zimepokewa tofauti za athari na daraja za swaumu, wanachuoni wa Akhlaq wamegawa swaumu katika sehemu tatu, ambazo ni:

Kwanza: Swaumu Khaasu Alkhaasu: nayo ni kufunga kwa moyo, akili na viungo vyote katika mambo ya siri na ya wazi, kujizuia na maasi ya duniani na fikra za kidunia za mambo yote yaliyo haramishwa na Mwenyezi Mungu, ukitafakari mambo ya dunia yawe ni mambo yanayo husu duni, kufanya hivyo ndio kuandaa zawadi ya akhera, funga hiyo humzuia mtu kujishughulisha na kila jambo la haram.

Pili: Swaumu Khaasu: nayo ni swaumu yenye daraja la juu zaidi kushinda swaumu Aamu, pamoja na kuacha vifunguzi vya funga vilivyo tajwa katika Swaumu Aamu, hufunga viungo vyake kufanya madhambi, makuruhu na mambo yenye utata kisheria, na kila jambo lisilo pendeza kufanywa na mja mtiifu miongoni mwa kauli na vitendo, imepokewa kutoka kwa Imamu Swadiq (a.s) anasema: (Unapo funga uhakikishe yamefunga masikio yako, macha yako, nywele zako na ngozi yako…).

Kufunga kwa viungo kunamaanisha kuzuia kiungo chochote kisifanye jambo la haram, makuruhu au lenye utata, kama vile kuongea maneno yasiyo faa, kusikiliza utesi, kuangalia mambo ya haram na mengineyo.

Tatu: Swaumu Aamu: Nayo ni kujizuia na vifunguzi vya funga vilivyo tajwa katika vitabu vya fiqhi na rasaaili amaliyya za Maraajii, aina hii ya funga hufanywa na kila mwislamu balekhe, kwa ajili ya kutekeleza wajibu walio pewa na kutafuta thawabu na radhi za Mwenyezi Mungu mtukufu kwa kutekeleza maamrisho yake, mtu anaweza akafunga na akajizuia kufanya vitu vinavyo julikana kisheria kama vifunguzi vya swaumu lakini akawa anafanya mambo ya haram, kama vile kuangalia mambo yasiyo faa, kuteta na mengineyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: