Muendelezo wa maandalizi ya kongamano la kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s)…

Sehemu ya kongamano
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) awamu ya kumi na moja, imetangaza kua inaendelea na maandalizi ya kongamano litakalo anza mwezi kumi na nne Ramadhani hadi mwezi kumi na sita katika bustani za muujiza wa kurudisha jua (Radu shamsi) wa Imamu Ali (a.s) katika mkoa wa Baabil mji wa Hilla, chini ya kauli mbiu isemayo (Imamu Hassan –a.s- ni muokozi wa waislamu na mfichuaji wa uovu wa wanafiki), hii ndio program kubwa ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Hassan Almujtaba (a.s).

Kwa mujibu wa maelezo ya mjumbe wa kamati ya maandalizi na naibu rais wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Aqiil Abdulhussein Yasiri: “Kongamano linasimamiwa na kamati kuu ya mradi wa Hilla mji wa Imamu Hassan Almujtaba (a.s) kwa kusaidiana na ofisi ya wakfu shia katika mkoa wa Baabil chini ya ulezi wa Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya, hii ni awamu ya kumi na moja, kwa baraka za tunaye muadhimisha tunatarajia iwe bora zaidi na iendane na heshima yake na hadhi ya Ataba mbili tukufu”.

Akaendelea kusema kua: “Tumefanya kila juhuhudi na tumepitia mawazo tofauti kwa ajili ya kuhakikisha kongamano hili litakalo husisha shughuli ya kupandisha bendera ya Imamu Hassan (a.s) na maonyesho ya picha za Hashdi Sha’abi pamoja na vikao vya usomaji wa Qur’an na mashairi, sambamba na vikao vya mihadhara ya kitafiti ya kisekula na kihauza, pamoja na ratiba ya ufunguzi na ufungaji itakayo husisha utoaji wa matamko na usomaji wa mashairi na kaswida”.

Akabainisha kua: “Kuna program zitakazo fanyika pembezoni mwa kongamano hilo, kama vile kutoa zawadi kwa wanahabari na hafla ya kumkumbuka Alamah Shekh Ibun Idrisa Hilliy itakayo fanyika kwa kushirikiana na kituo cha turathi za Hilla kilicho chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu, pamoja na hafla nyingine itakayo fanywa na Atabatu Kadhimiyya kwa kushirikiana na kamati kuu ya mradi wa Hilla mji wa Imamu Hassan Almujtaba ikiwa ni pamoja na kutoa zawadi kwa familia za mashahidi wa fatwa ya kujilinda”.

Kumbuka kua kongamano hili ni miongoni mwa makongamano makubwa ambayo hufanywa kila mwaka kwa ajili ya kuadhimisha kuzaliwa kwa Imamu Hassan (a.s) na linalenga kuonyesha nafasi aliyo kua nayo Imamu (a.s), na kubainisha msimamo wake dhidi ya mtawala wa kipindi chake ambaye ni Muawiya, pamoja na kuangazia mitihani na mateso aliyo pata Imamu (a.s) katika maisha yake, na kujikumbusha baadhi ya usia wake na hadithi za malezi na maelekezo ya Imamu katika maadili mema na siri za ibada, na kuifanyia kazi misingi ya ubinadamu aliyo kua nayo (a.s) inayo endana na maendeleo ya kijamii ya sasa.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: