Leo: Akhamisi ya pili katika mwezi mtukufu wa Ramadhani (11439h).
Sehemu: Haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Tukio: Ziara ya usiku wa Ijumaa.
Hakika Mwenyezi Mungu mtukufu kila siku ya mwezi wa Ramadhani wakati wa futari huwa acha huru na moto watu milioni moja, sasa hali itakuaje unapo kua mahala palipo tukuzwa na Mwenyezi Mungu, katika malalo ya bwana wa mashahidi Imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Ataba mbili tukufu Husseiniyya na Abbasiyya zimepokea makundi ya mazuwaru wanaokuja kutoka mikoa tofauti kuhuisha usiku wa pili wa Ijumaa katika mwezi mtukufu wa Ramadhani ndani ya haram tukufu ya bwana wa mashahidi na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
Kama kawaida ya watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), wanatoa huduma bora kwa mazuwaru watukufu, kila mmoja kutokana na kitengo chake na kwa mujibu wa majukumu aliyo pangiwa, wakisukumwa na lengo moja kuu ambalo ni: kumtumikia zaairu aliye funga ni utukufu kwetu, na kupata radhi za Mwenyezi Mungu mtukufu na radhi za mwenye malalo hii tukufu Abulfadhil Abbasi (a.s) ndio lengo letu, utawaona wanashindana kutoa huduma kuanzia sehemu za nje hadi katika malalo tukufu.