Vikao vya usomaji wa Qur’an vinafanywa kila siku na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) katika ukumbi wake mtukufu…

Sehemu ya kikao cha usomaji wa Qur’an
Atabatu Abbasiyya tukufu tangu ulipo ingia mwezi wa rahma na maghfira ambao ni mwezi wa Qur’an inashuhudia harakati kubwa za Qur’an, zinasomwa aya tukufu za Qur’an kwa ajili ya kuondoa kutu katika nyoyo zetu, zinafanyika harakati mbalimbali za Qur’an tukufu, kuanzia mahafali, vikao vya usomaji wa Qur’an, mashindano na nadwa kuhusu Qur’an, ikiwa ni pamoja na vikao vya usomaji wa Qur’an vinavyo fanywa na watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) asubuhi ya kila siku katika ukumbi wake mtukufu na hushiriki mazuwaru pia.

Katika kikao cha usomaji wa Qur’an, husomwa juzuu moja kila siku na idadi kadhaa ya washiriki wa kikao hicho, pamoja na kusherehesha baadhi za aya zinazo hitaji kushereheshwa miongoni mwa aya zilizo somwa, pia washiriki wanaruhusiwa ya kumsahihisha msomaji anapo kosea, hivyo ni vikao vya usomaji, tafsiri na kujifunza, vinaendelea hadi mwisho wa mwezi huu mtukufu.

Wasimamizi wa vikao hivi wamesema kua, harakati yeyote inayo husu kitabu cha Mwenyezi Mungu mtukufu, inafaida za kidini na ki-akhlaq, na inafaida ya kuwaimarisha watumishi na mazuwaru katika usomaji sahihi, na kwa upande mwingine ni fursa ya kunufaika na mwezi huu mtukufu na kupata radhi za Mwenyezi Mungu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: