Maboresho mapya yamejumuisha:
- 1- Zimeongezwa sauti za dua za kila siku katika nakala za maandishi za zamani.
- 2- Zimeongezwa sauti za ziara za Maimamu (a.s) za siku za wiki katika nakala za maandishi za zamani.
- 3- Zimeongezwa sauti za dua za baada ya swala za faradhi katika nakala za maandishi za zamani.
- 4- Zimeongezwa sauti za dua za wasomaji wapya.
- 5- Imeongezwa Qur’an iliyo somwa na Muhammad Swidiq Minshawi katika maktaba ya wasomaji waliokuwepo zamani.
- 6- Kimeongezwa kipengele maalumu cha dua.
Matokeo ya uboreshaji huu, kumekua na ongezeko kubwa la watumiaji wa ndani na nje ya Iraq, watumiaji wa kila siku ndani ya siku tisa za kwanza katika mwezi wa Ramadhani ni zaidi ya (9,000,000) milioni tisa. sawa na wastani wa watumiaji (1,000,000) kila siku.
Kumbuka kua aprication hiyo inapatikana katika (Google Play) na unaweza kuipakua kupitia (App Store).
Ukitaka kuipakua kupitia mtandao wa kimataifa Alkafeel tumia anuani hii:
https://alkafeel.net/Apps/Mcb/